Mshukiwa wa mashambulizi mawili
ya mabomu mjini Abuja ,nchini Nigeria, ambayo yaliwaua watu 75 ,
amerejeshwa nchini Nigeria kutoka Sudan.
Boko Haram ni nani?
- Boko Haram lilibuniwa mwaka 2002.
- Nia na lengo la kundi hilo ilikuwa kupinga elimu ya kimagharibi.
- Lilianza kufanya mashambulizi mwaka 2009
- Maelfu wameuawa hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
- Kundi hilo pia limeshambulia makao makuu ya UN mjini Abuja
- Takriban watu milioni 3 wameathirika
- Kundi hilo lilitangazwa kuwa la kigaidi na Marekani mwaka 2013
Anatuhumiwa kwa kupanga mashambulizi yaliyofanyika katika kituo cha basi mapema mwaka huu ambayo Boko Haram ilikiri kuyafanya.
Maelfu ya watu wameuawa nchini Nigeria mwaka huu peke kutokana na mashambulizi ya Boko Haram wakitaka kuruhusiwa kuunda jimbo lenye kufuata sheria za kiisilamu Kaskazini mwa nchi.
No comments:
Post a Comment