Mwanamme mmoja kutoka Marekani
amedai umiliki wa kipande kidogo cha ardhi barani Afrika kama ufalme
wake kwa sababu bintiye anataka kuwa binti mfalme.
Jeremy Heaton aliambia BBC kuwa amesafiri kutoka
Virginia nchini Marekani na bendera yake kutangaza eneo hilo kwa Ufalme
wa 'Sudan Kaskazini.'Eneo hilo ni jangwa la mraba wa maili 800 lililo kati ya Misri na Sudan, na halijamilikiwa na nchi yoyote.
Alisema kuwa ameandikisha rasmi maombi kwa nchi hizo mbili, japo bado hajapa jibu.
“Kama babake, nilitambua kuwa ombi lake halikuwa mzaha, ” Heaton alisema.
“Nilitafiti vipande vya ardhi visivyomilikiwa na nikabahatika kuvigundua.”
Ili kuadhimisha miaka misaba tangu kuzaliwa kwa bintiye, Heaton alisafiri kwenda panapofahamika na wenyeji kama ‘Bir Tawil’ ili kutimiza ombi la Emily.
Heaton ambaye ana watoto watatu alisema kuwa angefanya lolote ili kudhibitishia wanawe kuwa anaweza kuenda “kokote kwa ajili yao.”
Tarehe 16, mwezi Juni, Heaton aliwasili jangwani na kuweka bendera iliyochorwa na bintiye, na kusisitiza madai yake ni halali.
Mzozo wa mipaka kati ya nchi ya Sudan na Misri unaashiria kuwa jangwa hilo ni kati ya vipande vya mwisho duniani visivyomilikiwa
Tofauti, anavyosema, ni kuwa aghalabu vita huzuka ili kupata umiliki huo, bali kwa kesi yake, “kuanzisha nchi hiyo ni ishara ya mapenzi yake kwa bintiye.”
Hata kama hakuna uwezekano kuwa Jeremy Heaton atakuwa mfalme wa nchi hiyo mpya ya Sudan kaskazini, ana mipango atakavyoendeleza “nchi hiyo.”
Binti mfalme Emily, aitwavyo sasa na familia yake, ametoa amri ardhi yake mpya iwe kituo cha ukulima. Sasa anavalia nguo za kimalkia na taji yake ya kifalme popote aendapo na anasema “inampendeza” kuwa binti wa mfalme, lakini bado hajafahamu ni lini atakapozuru anachofikiria kuwa nchi mpya zaidi ulimwenguni.
Itabidi Misri, Sudan na Umoja wa Mataifa kutambua 'Ufalme wa Sudan' kabla hajakuwa rasmi bintiye mfalme.
No comments:
Post a Comment