Baadhi ya wananchi wa Kata
ya Chumbi “A”, Tarafa ya Muhoro,Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani wakifuatilia kwa umakini hafla fupi ya kukabidhi baiskeli kutoka UMATI kwa wahudumu wa Afya ya uzazi ngazi ya jamii, iliyofanyika katika Kata hiyo, Ijumaa
Mei 30, 2014.
Baadhi ya wahudumu wa Afya ya uzazi ngazi ya jamii wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kukabidhiwa baiskeli kutoka
UMATI katika hafla fupi iliyofanyika Ijumaa, Mei 30, 2014 katika Kata ya Chumbi “A”
Wilaya ya Rufiji, Mkoani Pwani.
Baadhiyawananchiwa Kata
yaChumbi “A”
Tarafa ya Muhoro Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani wa kifuatilia kwa umakini hafla fupi ya kukabidhi baiskeli kutoka
UMATI kwa wahudumu wa Afya ya uzazi ngazi ya jamii iliyofanyika katika Kata hiyo, Ijumaa, Mei 30, 201.
Baadhi ya wananchiwa Kata
ya Chumbi “A”
Tarafaya Muhoro Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani wakifuatilia kwa umakini hafla fupi ya kukabidhi baiskeli kutoka 'UMATI" kwa wahudumu wa Afya ya uzazingazi ya jamii iliyofanyika, kakatika, Kata hiyo, Ijumaa
Mei 30, 2014.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani,
Rasmo Msabaha (aliyesimama), akizungumza na wananchi waliohudhuria Katika hafla fupi ya kukabidhi baiskeli kutoka
UMATI kwa wahudumu wa Afya ya uzazi ngazi ya jamii katika hafla fupi iliyofanyika Ijumaa, Mei
30, 2014 katika Kata ya Chumbi “A” Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani. (Picha zote na MAELEZO)
Na Ismail Ngayonga
MAELEZO, RUFIJI
Mei 30, 2014
CHAMA
cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), imewapatia baiskeli 40 zenye thamani ya Tsh.
Milioni 4.8 wahudumu wa afya ya uzazi na ujinsia ngazi ya jamii waliopokatika Kata
za Chumbi “A” na Bunguzi ilizopo Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.
Akizungumza Wilayani hapa Ijumaa
(Mei 30, 2014), Mkurugenzi Mtendaji, wa UMATI, Bi. Lulu
Ng’wanakilala Katika hotuba yake ili yosomwa na Meneja Miradiwa UMATI, Bi. Tausi Hassan
alisema, lengo la kukabidhi baiskeli hizo, nijitihada za taasisi hiyo katika kushiriki ana na Serikali kuboresha ili kuboresha afya ya
mama na mtoto na kuhakikisha huduma bora zinapatikana kwa Mama
na Mtoto kabla na baadaya kujifungua.
Bi. Ng’wanakilala alisema
UMATI kupitia ufadhili washirika la MERCK Sharp and Dohme (MSD) kutoka nchini Marekani ili liweze kupata mradi wa uwiano katika ubunifu wa kuboresha Afya ya
Mama na Mtoto, mradi unaotekelezwa katika kipindi cha
miaka mitatu katika mikoaya Pwanina Katavi na kushirikiana kwa karibu zaidi na Ofisi za Mganga Mkuu wa Wilaya.
“Kwa Mkoa wa Pwani mradi huu unatekelezwa katika Wilaya ya Rufiji katika
Kata ya Chumbina Bungu na utekelezaji wake katika maeneo husika ulianza mwaka jana (2013) na miongoni mwa kazi za mradi ni mikutano elimishi kwa jamii,
mafunzo ya waelimisha rika, mafunzo kwa wahudumu ngazi ya jamii” alisema Bi. Ng’wanakilala.
Aidha, alisema mpaka sasa yapo mafanikio yaliyokwishapatikana tangu kuanza mradihuo katika Mkoa wa Pwani,
hususani Wilaya ya Rufiji ambapo miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na wahudumu 40
ngazi ya jamii wamepatiwa mafunzo na kuanza kazi ya kuhudumiajamii.
Aliyataja mafanikio mengine ni kuwa ni pamoja na vijana
20 waelimishajirika katika ushiriki wa wanaume masuala ya uzazi na uzazi salama walipatiwa mafunzo na kuanza kutoa elimukwajamii.
Jamii imeweza kuupokea mradivi zuri na kuonesha ushirikiano kutoka ngazi ya jamii, Serikali ya Kata/kijiji husika mpaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya.
Jamii imeweza kuupokea mradivi zuri na kuonesha ushirikiano kutoka ngazi ya jamii, Serikali ya Kata/kijiji husika mpaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya.
Kwamujibu wa Ng’wanakilala alisema katika mradi huo zipo changamoto mbalimbali zikiwemo baadhi ya wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kuacha kazi,
upungufu wa rasilimali katika utekelezaji wa mradi pamoja na Mabadiliko ya haliyahewa na tabianchi ikiwemo mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni nchini ambapo zilileta uharibifu wa miundombinuyabarabaranamadaraja.
Kwaupande
wake Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Bw. Rasmo Msabaha alisema Mkoa huo umepanga kufikia asilimia
60 ya malengo iliyojiwekea katika kuzuia vifo vya Mama
na Mtoto na hadi kufikia sasa umefikia asilimia 37,
na hivyo jitihada za pamoja hazina budi kufanywa katika kufikia kiasi kilichobaki.
“Uzazi wa Mpango ni muhimu sana,
hapo zamani Serikali iliweza kutoa bure huduma za afya na elimu,
lakini kwasasa idadi ya wananchi imekuwa kubwa na ndio maana Serikali imeamua kushirikiana na sekta binafsi ikiwemo UMATI ili kuweza kusaidia huduma za afya, hivyo ni lazima tuzae kwa mpangilio na kwa kadri tunavyoweza kuwahudumia”
alisema
Aidha, Msabaha alisema kuwa Ofisi yake imejipanga kikamilifu katika kushirikiana kwa karibu zaidi na wahudumu wa afya ya uzazi ngazi ya jamii waliopatiwa mafunzo na
UMATI ili kuhakikisha kuwa malengo ya mradi huo yanafikiwa kwa wakati na muda uliopangwa.
Kwamujibu wa Msabaha aliwataka Wahudumu wa afya ya uzazi kuzingatia mafunzo waliyopatiwa na
UMATI
na kufanyakazi walizoelekezwa na Ofisi yake ipotayari kupokea taarifa ya utelezaji wa mradi huo naendapo kutakuwepo na tatizo lolote Ofisi hiyo ipotayari kutoa ushirikiano kwa kadri inavyowezekana.
Naye Diwaniwa
Kata ya Bungu, Bw. Ramadhani Mkwaya alisema Ofisi yake imeupokea kwamoyo mmoja mradi huo na ipotayari kuutekeleza,
na akaishukuru UMATI kuichagua Kata yake kati ya Kata 27 zilizopo katika Wilaya hiyo na kusema kuwa hicho ni kielelezo kuwa
Kata hiyo, inakubalika kimaendeleo.
Aidha, Diwani wa
Kata ya Chumbi,Bw. Ramadhani Mikole aliwataka wahudumu hao wa afya ya uzazi ngazi ya jamii kutokuwa kimya iwapo kutatokea tatizo
la kiutendaji katika majukumu yao,
na badala yake wawasiliane mara moja na wahusika wa mradi ili kuhakikisha kuwa mradi unafikia malengo yake.
“Elimu ya siku
9, mliyopewa ni nzuri na pia nichangamoto, iwapo program inaruhusu na waombeni UMATI
muongeze tena siku 9 kwani wahudumu hawa wanafanya shughuli nyingi sana” alisema Mikole.
Mwakilishi wa Shirika
la Merck Sharp and Dohme (MSD), Bw. John Nkane alisema shirika hilo ni kampuni ya dawa inayojihusisha zaidi na masuala yabiandamu na imejitolea katika kupambana na vifo vya akina
Mama vitokanavyo na uzazi na wameshirikiana na UMATI
na kufadhili mradi huo, ikiwemo kutoa elimu kwa akina Mama
kuhusu umuhimu wa kuhudhuria kliniki.
“Taarifa zilizopo ni kwamba baadhi ya Akina Mama Wajawazito wanakwenda maeneo yasiyorasmi, na hivyo shirika letu limejitolea katika kusaidia kuokoa uhai wa Mama na Mtoto, na tumetoa pesa, elimu na kutoa mada mbalimbali” alisema.
No comments:
Post a Comment