Mwenyekiti wa malezi Youth Theatre Kituo cha vijana UMATI Bi.
Asha Chande akiwapa ujumbe mfupi vijana na watoto waliohudhuria Tamasha hilo
kuhusu namna ya Tamasha litakavyoendeshwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
Afisa Msaidizi wa Vijana kituo cha UMATI tawi la Dar es
Salaam Bi. Upendo Daud akiwaeleza vijana kuhusu mada kuu ya Tamasha ambayo ni
“Athari za ndoa za utotoni” wakati wa ufunguzi wa tamasha la mwezi katika kituo
hicho.
Mwenyekiti wa mtaa wa Wailes Bw. Abdul Kidege ambaye ndiye mgeni
rasmi katika Tamasha la Jamvi la vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam
akitoa hotuba yake fupi kwa vijana waliohudhuria tamasha hilo lenye lengo la
kuwaeleimisha vijana juu ya athari za ndoa za utoton
Mwenyekiti wa mtaa wa Wailes Bw. Abdul Kidege ambaye ndiye mgeni
rasmi katika Tamasha la Jamvi la vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam
akitoa hotuba yake fupi kwa vijana waliohudhuria tamasha hilo lenye lengo la
kuwaeleimisha vijana juu ya athari za ndoa za utoton
Vijana wakifatilia kwa makini hotuba ikiyotolewa na mgeni
rasmi kabla ya ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana Kituo cha UMATI jijini
Dar es Salaam.
Vijana wakifatilia kwa makini hotuba ikiyotolewa na mgeni
rasmi kabla ya ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana Kituo cha UMATI jijini
Dar es Salaam.
Watoto wadogo wakitoa burudani mbele ya mgeni rasmi
wakiongozwa na Bw. Mzome (aliyeshika kipaza sauti) ambaye ni mmoja kati ya
vijana waigizaji katika kundi la Malezi Theatre tawi la Dar es Salaam.
Baadhi ya vijana waliohudhuria Tamasha wakiwaangalia watoto
wakicheza muziki wakati wa tamasha la Jamvi la Vijana kituo cha UMATI jijini
Dar es Salaam.
Vijana kutoka kundi la YAM wakitoa burudani mbele ya mgeni
rasmi wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana kituo cha UMATI jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa mtaa wa Wailes Bw. Abdul Kidege (kushoto)
akifatilia kwa makini michezo ya maigizo toka kwa vijana wa kundi la The Africa
wakati wa Tamasha la Jamvi la Vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Afisa Msaidizi wa Vijana kituo cha UMATI Bi. Upendo Daud.
Vijana, watoto pamoja na watu wazima wakifatilia kwa makini
maigizo toka Kundi la The Africa wakati wakitoa burudani mbele ya mgeni rasmi
(hayupo pichani)
Vijana, watoto pamoja na watu wazima wakifatilia kwa makini
maigizo toka Kundi la The Africa wakati wakitoa burudani mbele ya mgeni rasmi
(hayupo pichani)
Kijana ambaye ni mwanafunzi Shule ya Sekondari ya Wailes
Zahoro Muhidini akitoa burudani mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) yenye
ujumbe mzuri unaowahusu vijana kujiepusha na ndoa za utotoni na maambukizi ya
virusi vya Ukimwi wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana kituo cha
UMATI jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa kituo cha UMATI tawi la Dar es Salaam
wakiwaeleza na kuwauliza maswali vijana na watoto juu ya kitu walichojifunza
wakati wa tamasha la Jamvi la Vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam.
Vijana toka kundi la The Africa wakionesha igizo maalum
linalohusu athari ya maradhi mbalimbali yakiwemo TB na Ukimwi yanayoweza
kuwakumba vijana katika maisha yao ya ujana endapo hawatakuwa makini na jinsi
gani ya kujiepusha nayo.
Vijana toka kundi la The Africa wakionesha igizo maalum
linalohusu athari ya maradhi mbalimbali yakiwemo TB na Ukimwi yanayoweza
kuwakumba vijana katika maisha yao ya ujana endapo hawatakuwa makini na jinsi
gani ya kujiepusha nayo.
Wakubwa kwa wadogo wakifatilia moja ya maigizo toka kwa kundi
la The Africa yenye kuwapa vijana elimu juu ya ndoa za utotoni, namna ya kujikinga
dhidi ya maradhi na kukemea tabia za baadhi ya wazazi kuwalazimisha vijana wao
wa kike kuolewa katika umri mdogo.
Mshereheshaji (DJ) akiwa kazini kuwapa burudani vijana
waalikwa pamoja na watoto waliohudhuria Tamasha la Jamvi la Vijana kituo cha
UMATI jijini Dar es Salaam.
Vijana wa kundi la The Africa wakiendelea kutoa elimu kwa
njia ya maigizo mbele ya vijana wenzao (hawapo pichani) wakati wa la Jamvi la
Vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam.Vijana wa kundi la The Africa wakiendelea kutoa elimu kwa njia ya maigizo mbele ya vijana wenzao (hawapo pichani) wakati wa la Jamvi la Vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam.
Vijana wa kundi la The Africa wakiendelea kutoa elimu kwa njia ya maigizo mbele ya vijana wenzao (hawapo pichani) wakati wa la Jamvi la Vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam.
Vijana wa kundi la The Africa wakiendelea kutoa elimu kwa
njia ya maigizo mbele ya vijana wenzao (hawapo pichani) wakati wa la Jamvi la
Vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo, Dar es Salaam)
Na Benedict
Liwenga-MAELEZO, Dar es Salaam
NDOA nyingi za utotoni husababishwa na tabia ya baadhi ya
wazazi na walezi kuwalazimisha watoto wao wa kike kuolewa katika umri mdogo kwa
tamaa ya kujipatia fedha ama utajiri katika familia zao jambo ambalo
linawanyima haki ya kusoma watoto wengi kwani watoto hawa wanakuwa wako katika
umri chini ya miaka kumi na nane.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Wailesi Wilaya ya
Temeke Bw. Abdul Kidege wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana
linalofanyika kila mwisho wa mwezi katika kituo cha vijana UMATI jijini Dar es
Salaam.
Bw. Kidege amesema kuwa kuna baadhi ya wazee na vijana wenye
tabia ya kuwarubuni wasichana wadogo kwa kuwapa pesa na vitu vya thamani kwa
lengo la kuwashawishi kuolewa nao na pia kuna baadhi ya wazazi ambao wakati
mwingine ushirikiana katika kufanikisha azma hiyo jambo ambalo ni kinyume na
haki za watoto katika jamii.
“Kuna baadhi ya wasichana wenye umri mdogo wamekuwa wakinyanyaswa
kijinsia kwa kubakwa na wengine kulazimishwa na wazazi wao wenyewe kuolewa na
watu wazima ambao wamewazidi umri, jambo hili halikubariki na vijana nawaasa
msikubali kurubuniwa kwa pesa au vitu toka kwa watu wa namna hiyo”. Alisema Bw.
Kidege.
Kwa upande wake Afisa Vijana Msaidizi Chama cha Uzazi na
Malezi Bora Tanzania (UMATI) Bi. Upendo Daud amewaeleza vijana waliohudhuria
tamasha hilo kuwa vijana wanapohudhuria matamasha katika kituo cha UMATI
wanapata fursa kubwa ya kupata elimu bure juu ya afya ya uzazi, athari za mimba
za utotoni, kupima Ukimwi, ushauri nasaha, uzazi wa mpango pamoja na
uelimishaji rika jambo ambalo linawafanya vijana wengi waweze kujitambua na
kujikinga.
“Hili ni Tamasha
kwaajili ya vijana linaloandaliwa kila mwisho wa mwezi na Youth Action Movement
(YAM) kwa lengo la kuwaelemisha vijana juu ya mambo mbalimbali yanayohusiana na
afya na mada kuu ya tamasha hili kwa leo ni Ndoa za umri mdogo na athari
zake”. Alisema Bi. Upendo.
Youth Action Movement (YAM) ni kikundi cha Vijana ambacho
kilianzishwa na chama cha uzazi na malezi bora Tanzania (UMATI) kwa ufadhili wa
Internationa Planned Parenthood Federation (IPPF). Chama hiki cha vijana
kinapatikana katika kila tawi la UMATI nchi nzima na kwa tawi la Dar es Salaam
ndiyo waandaaji wa Jamvi la vijana kila mwezi ambapo husaidia kutoa huduma bure
kwa vijana kuhusu afya ya uzazi, kupima Ukimwi, ushauri nasaha, uzazi wa mpango
pamoja na uelimishaji rika.
No comments:
Post a Comment