TANGAZO


Sunday, June 1, 2014

Kinana afunika mkutano wa Kiteto leo

 *Akagua miradi ya maendeleo ya wananchi

*Mamia wafurika mkutano wake mjini Kibaya

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa michezo mjini Kibaya wilayani Kiteto mkoani akiwa katika ziara yakea ya kukagua uhai wa Chama na kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia ya kuzitatua mkoani  Manyara leo, Mei 31, 2014.
 Katibu wa NEC, Ituikadi na Uenezi Nape Nnauye akiuunguruma kwenye mkutano huo uliofanyika Uwanja wa michezo mjini Kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara
 Mbungr wa Kiteto Benedict Ole Nangolo alivyosimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo hilo, baada ya kuitwa na Kinana kwenye mkutano huo
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo mjini Kibaya, Kiteto
Kinana (kushoto) akisamsalimia kwa kumgusa kichwani mmoja wa binti wa Kimasai, aliyeuangana na wananchi wa Kijiji cha Kimotoro, Simanjiro, aliposimama kwa muda akiwa anjiani kwenda wilayani Kiteto leo
 Kinana akiwasalimia wananchi kwenye mapokezi katika Kijiji cha Irkiushbor, Kiteto
 Kinana akimtwisha ndoo ya maji, Nangeriya Umbula, wakati akizindua mradi wa maji safi katika kijiji cha Eseki, Kiteto, leo Mei 31, 3014
 Nape akinywesha maji ng'ombe baada ya Kinana kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Eseki, Kiteto, leo Mei 31, 2014
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akipanda mti kwenye shule ya msingi Laakir, iliyopo kata ya Nalangtomon, Kiteto leo Mei 31, 2014.
 Majengo ya Shule ya msingi Laakir, Nalangtomon, Kiteto, ambayo mwaka jana iliongoza katika matokeo ya mitihani darasa la saba mkoa wa Manyara.
Nangeriya Nangoro wa Kijiji cha Laalakir, Kiteto, akimnywesha maziwa mtoto wake kwa kutumia kibuyu maalum, wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Kijiji hicho, alikokwenda kuzindua mradi wa maji, leo Mei 31, 2014. (Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog)

No comments:

Post a Comment