*Wambura, Juma Pinto, Asha Kigundula wasindikizwa kwa shangwe na maandamano
Asha Kigundula akijiandikisha kuchua fumo za kugombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba katika uchaguzi utakaofanyika mwishoni mwa mwezi wa Juni. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Asha Kigundula akikabidhiwa fumo za kugombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba katika uchaguzi utakaofanyika mwishoni mwa mwezi wa Juni na Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Khalid Kamguna (kushoto), Dar es Salaam leo.
Asha Kigundula akizionesha kwa waandishi wa habari fomu zake za kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba.
Asha kigundula akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hizo.
Bundala Kabulwa (kulia), akikabidhiwa fomu za kuwania uongozi wa Klabu ya Simba na Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi, Khalid Kamguna.
Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba, Khalid Kamguna (kushoto), akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, mwanachama Juma Pinto, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, watoaji wa Magazeti ya Jambo Leo, Jambo Brand na Staa Spoti kwa ajili ya uchaguzi Mkuu utakaofanyika Juni 29, mwaka huu.
Juma Pinto akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurejesha fomu za kuwania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifurahia jambo wakati Juma Pinto alipokuwa akizungumza katika hafla hiyo.
Juma Pinto akiondoka kwenye Klabu ya Simba mara baada ya kuzirejesha fomu zake za kuwania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo leo.
Juma Pinto (katikati), akizungumza na mashabiki wake mara baada ya kuzirejesha fomu za kuwania uongozi wa klabu yake ya Simba leo.
Mashabiki wa mwanachama Michael Wambura wakiwa kwenye maandamano na mgombea wao wakati alipokuwa akizirejesha fomu zake za kuwania Urais wa klabu hiyo jijini leo.
Mashabiki wa mwanachama Michael Wambura wakiwa kwenye maandamano na mgombea wao, huku wakiwa wamebeba mabango ya kuwakejeli wagombe wengine katika kinyanganyiro cha uongozi wa klabu hiyo jijini leo.
Mashabiki wa Klabu ya Simba wakiwa kwenye maandamano ya kumsindikiza mgombea wao wa Urais wa klabu hiyo.
Gari lililombeba Michael Wambura likiwa kwenye maandamano hayo.
Hili ndilo gari lililombeba Michael Wambura katika msafara wake wa kurejesha fomu za kuwania nafasi ya Urais wa Klabu ya Simba jijini leo.
Mashabiki na wananchama wa Klabu ya Simba wakiwa kwenyye maandamano hayo.
Muichael Wambura akiwapungia wananchi wakati wa kurejesha fomu zake jana.
\\\\michael Wambura akipeana mkono na mashabiki wake.
\wambura akiwasalimia mashabiki wake waliokuwa wakimsindikiza kwenda kurejesha fomu za kuwania nafasi ya Urais wa Klabu hiyo leo.
Wambura (kulia), akiwapungia mashabiki wake wakati wa kurejesha fumo zake leo.
Michael Wambura akiwa na mwanachama na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelu, wakati wa kurejesha fomu zake za kuwania Urais wa klabu hiyo leo.
Michael Wambura akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuzirejesha fomu za kuwania Urais wa klabu hiyo leo.
Mwanachama wa Klabu ya Simba, Michael Wambura (kulia), akikabidhi fomu za kuwania nafasi ya Rais kwa Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Khalid Kamguna, wakati alipozirejesha baada ya kuzijaza klabuni hapo leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo leo klabuni hapo.
Jamhuri akihesabu fedha zake kabla ya kuzikabidhi kwa Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi leo.
Mwanachama,kocha na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelu (kulia), akilipia fomu za kuwania nafasi ya Makamu wa Rais kwa dola za Marekani kwa Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Khalid Kamguna (kushoto) katika Makao Makuu ya klabu hiyo, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam leo.
Mwanachama,kocha na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelu (kulia), akilipia fomu za kuwania nafasi ya Makamu wa Rais kwa dola za Marekani kwa Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Khalid Kamguna (kushoto) katika Makao Makuu ya klabu hiyo, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam leo.
Mwanachama,kocha na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelu (kulia), akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Makamu wa Rais na Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Khalid Kamguna.
Jamuri kihwelu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu za kuwania Makamu wa Rais wa klabu hiyo jijini leo.
Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari, wakiwa katika klabu hiyo kufuatilia uchukuaji fomu za kuwania uongozi wa klabu hiyo leo.
Wambura akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzirejesha fomu zake za kuwania Urais wa klabu hiyo leo.
Wambura akiongea katika hafla hiyo leo.
Mwanachama na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Simba, Arthur Mambeta (kulia), akizungumza kabla ya kumkabidhi kombe mgombea wake katika uchaguzi huo.
Mwanachama wa Klabu ya Simba, Wambura (kushoto), akikabidhiwa kombe na mmoja wa wanachama na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Arthur Mambeta mara baada ya kurejesha fomu za kuwania Urais wa klabu hiyo leo kwa Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Khalid Kamguna.
Haya ni Baadhi ya mabango yaliyomsindikiza mgombea wa nafasi ya Urais, Wambura.
No comments:
Post a Comment