Kaimu
mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Bw. John Muya akiwaeleza
waandishi wa habari mafanikio yaliyofikiwa
na Mfuko huo katika Kupambana na
Ujangili katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Na Georgina
Misama-MAELEZO
MFUKO wa Kuhifadhi
Wanyamapori Tanzania (TWPF) umebuni miradi ya maendeleo kama vyanzo vya mapato
ili kukabiliana na changamoto ya ufinyu wa bajeti katika kutekeleza majukumu
yake.
Hayo yamesemwa na Kaimu
Mtendaji Mkuu wa mfuko huo Bw John Muya wakati wa mkutano na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo.
Alisema kwamba mfuko
umebuni miradi ya maendeleo ili kujiendeleza kwa kuongeza mapato ambapo alitaja
miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa Jengo la Kakakuona na Pori la akiba la Pande.
Miradi mingine ni
Bustani ya Wanyamapori ya Tabora, Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila-Songea na
kambi ya Utalii katika Pori la akiba Selous.
Muya alisema TWPF
husimamia ukusanyaji wa maduhuli, usimamizi wa uwindaji wa kitalii na wa
wenyeji, utalii wa picha, biashara ya wanyamapori hai na mazao yatokanayo na
wanyamapori, mashamba na bustani za ufugaji wa wanyamapori.
Kwa upande wake Kaimu Katibu
Tawala wa TWPF Bi. Antonia Raphael alisema mfuko hugharamia shughuli mbalimbali
za usimamizi wa wanyamapori ikiwa ni
pamoja na usimamizi wa maeneo ya jumuia za hifadhi za wanyamapori (WMAs), kutoa
elimu ya uhifadhi kwa jamii na uendelezaji wa miundombinu katika mapori ya
akiba.
Mfuko hufanya malipo ya kifuta machozi kwa wananchi
ambao ndugu zao wameuawa au kujeruhiwa na wanyamapori ambapo kwa kipindi cha
miezi mitatu Januari –Machi 2014, kiasi cha shilingi milioni 9 kililipwa kwa
ajili waliouwawa.
No comments:
Post a Comment