Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa (kushoto) na Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wakifurahia jambo wakati wa
uzinduzi wa huduma ya M PAWA ambayo inamwezesha mteja kupata huduma za
kibenki kwenye simu ya mkononi kwa njia ya M-pesa iliyozinduliwa kwa
ushirikiano wa Vodacom Tanzania na Benki ya CBA, Dar es Salaam leo. Kupitia huduma hiyo
mteja wa M-pesa anaweza kuweka, kutoa na kukopa pesa.
Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Vodacom Tanzania Balozi Mwanaidi Maajar mara baada ya kuzindua huduma
mpya ya M-pawa ya kuweka pesa, kutoa na kukopa kwenye simu ya mkononi
kwa njia M-pesa kwa ushirikiano na Benki ya CBA jijini Dar es Salaam leo. Wa
kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CBA Tanzania Ndewirwa Kitomari Wengine
kutoka kushoto ni Naibu Mwenyekiti wa CBA Group Muhoho Kenyatta,
Mwenyekiti wa Bodi ya CBA Group Desterio Oyatsi, Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom Rene Meza.
Rais Jakaya Kikwete (wa tatu kushoto) akiwa pamoja na kutoka kushoto
Mwenyekiti wa CBA Tanzania Ndewirwa Kitomari, Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania Balozi Mwanaidi Maajar, Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Rene Meza, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa Bodi ya CBA Group
Desterio Oyatsi na Naibu Mwenyekiti wa CBA Group Muhoho Kenyatta mara
baada ya Rais kuzindua huduma mpya ya M-pawa ya kuweka pesa, kutoa na
kukopa kupitia simu ya mkononi kwa njia M-pesa kwa ushirikiano na Benki
ya CBA jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza kabla ya kuzindua rasmi huduma mpya ya
M-pawa ya kuweka pesa, kutoa na kukopa kupitia simu ya mkononi kwa njia
M-pesa inayotolewa kwa ushirikiano wa Vodacom Tanzania na Benki ya CBA
jijini Dar es salaam.
Dar
- es - salaam Mei 14, 2014
KAMPUNI kinara ya mtandao wa huduma za
mawasiliano ya simu za mkononi nchini Vodacom na Benki ya Biashara
Afrika - CBA leo wamezindua huduma mpya yenye kuleta mapinduzi makubwa
ya M-pawa itakayowawezesha mamilioni ya watanzania kuhifadhi fedha na
kukopa kupitia simu zao za mkononi.
Akizundua huduma hiyo jijini Dar
es Salaam Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alisema "Uzinduzi wa
kihistoria wa M-pawa kwa kiasi kikubwa ni uthibitisho wa mafanikio
yaliyotokana na mageuzi yaliyofanyika kwenye sekta ya fedha nchini
ambayo yamechangiwa pamoja na mambo mengine uwekezaji mkubwa katika
sekta ya mawasiliano na hivyo kuwawezesha wananchi kumudu kuzifikia
huduma za fedha."
"M-pawa ni ubunifu mpya katika sekta ya huduma za
fedha ambao unaleta pamoja uzoefu wa zaidi ya miaka 50 wa benki ya CBA
katika Afrika Mashariki na mafanikio makubwa ya mtandao mpana wa huduma
ya M-pesa wenye mawakala zaidi ya 65,000 nchi nzima.
Huduma hii
itaimarisha zaidi uletaji pamoja wa huduma za kifedha kwa kuwezesha
wananchi kuweka akiba ya hadi Sh. 1/-, na kukopa kadiri mteja
anavyokidhi vigezo."Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene
Meza.
"M-pawa ni rahisi kutumia, mteja haitaji kutuma wala kujaza
fomu za maombi. Kila mmoja sasa anaweza kufungua akaunti ya benki kwenye
benki ya CBA kwa urahisi zaidi kiasi tu cha kuchagua M-pawa kutoka simu
yake ya mkononi katika menu ya huduma ya M-pesa. Zaidi, haina gharama
zozote wala ukomo wa kutoa ama kuhamisha fedha kutoka M-pesa kwenda
M-pawa na kinyume chake"Alisema Meza.
"M-pesa ilikuwa ni mbia sahihi
kwetu kuifikisha huduma hii Tanzania tukiamini kuwa kupitia mtandao
wake mpana na mfumo imara wa mawakala zaidi ya 65,000 waliosambaa nchi
kote, huduma hii itapokelewa na kukua kwa kasi hapa nchini."Alisema
Mwenyekiti wa Bodi ya CBA Tanzania Ndewirwa Kitomari.
Vodacom na
CBA inalenga kuwafikia mamilioni zaidi ya watanzania walio nje ya mfumo
rasmi wa huduma za kibenki nchini mbali na wateja Milioni 5 ambao tayari
kwa sasa wanatumia huduma ya M-pesa.
"Tunamatumaini ya kwamba
huduma hii itastawi hapa nchini kwa sababu tafiti mbalimbali zinaonyesha
kwamba wananchi wengi wanapenda kuweka akiba ili kustawisha maisha yao
lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa kukosa sifa na vigezo vya benki,
M-pawa inatoa jawabu la mahitaji hayo."Alisema Meza.
Ili mteja
ajiunge na huduma ya M-pawa anachopaswa kufanya ni kuchagua M-pawa
kutoka kwenye menu ya M-pesa na halafu kuchagua huduma kulingana na
mahitaji yake kwa wakati huo kama vile kuweka akiba, kutoa ama kuomba
mkopo.
"Kwa upande wa huduma ya mikopo, mteja wa Vodacom anapaswa
awe ametumia huduma ya M-pesa kwa kipindi cha miezi 6 na kuwa na awe na
akiba kwenye akaunti yake ya M-pawa."Amefafanua Meza.
Mbali na ubia na
CBA, M-pesa pia ina ubia wa kibiashara na benki zaidi ya 21 hapa nchini
inayowapa uwezo wateja wake kuweka ama kutoa fedha wakati wowote mahali
popote kwa urahisi zaidi katika akaunti walizonazo kwenye benki hizo.
Aidha, kwa sasa huduma ya M-pesa ndio chaguo la kwanza la malipo ikiwa
imeunganishwa na malipo ya huduma zaidi ya 200 nchini Tanzania na pia
kunufaisha biashara hizo.
No comments:
Post a Comment