Kampuni kubwa duniani ya vifaa
vye elektroniki, Samsung inasema kuwa itawalipa fidia wafanyakazi wake
waliougua Saratani kutokana na kufanya kazi katika viwanda vyake.
Kampuni hiyo iliomba radhi kwa kesi ya muda
mrefu kati yake na wafanyakazi hao waliokuwa wanadai fidia na badala
yake kukubali kujiondoa katika kesi hiyo huku ikikubali kuwalipa fidia
wagonjwa hao.Hatua ya Samsung kukubali kuwalipa wafanyakazi hao inaleta matumaini katika kukamilika kwa mvutano huo ambao ulionekana kukwama kwa muda mrefu
Lakini afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, Kwon Oh-hyun nusura kukiri kuwa kulikuwa sababu ya wafanyakazi hao kupatwa na Saratni ilichangiwa na wao kufanya kazi katika kiwanda cha Samsung. Wengi walipata Saratani ya damu au Leukaemia.
"tulipaswa kumaliza kesi hii kitambo sana na bila shaka tunahisi uchungu kwamba tulikosa kufanya hivyo, tunaomba radhi kwa hilo. ''
Akiongea na wandishi wa habari, Bwana Kwon alisema kuwa Samsung inatumai kuwa itaweza kumaliza kesi hii na kuweza pia kuwapa afueni wagonjwa na familia zao.''
Hata hivyo kampuni hiyo kubwa zaidi duniani ya simu za Smartphone haikusema idadi ya watu watakaolipwa fidia ingawa inaarifiwa ni watu 40 waliowasilisha malalamiko hayo huku kesi ikiendelea kwa zaidi ya miaka sita.
No comments:
Post a Comment