Wanajeshi wakiwaondoa raia wa Sudan Kusini kutokana na mapigano
yanayoendelea
Wakati juhudi zikizidi kuendelea za kujaribu kumaliza mapigano
Sudan Kusini, Msemaji wa Jeshi la Sudan Kusini amesema kuna matumaini madogo ya
kusitishwa kwa mapigano.
Kiongozi wa waasi Riek Machar amesema wapiganaji wake bado wanashikilia eneo
kubwa la Kaskazini mwa nchi, huku majeshi ya serikali yakisema yameukomboa mji
wa Malakal na wamezingira eneo la Bentiu , mji mkuu wa jimbo la Unity.
Rais Salva Kiir amesema yupo tayari kusitisha mapigano mara moja, lakini
hasimu wake Bwana Machar amesema mazungumzo zaidi yanahitajika kukubaliana
kusitisha mapigano na kwamba yupo tayari kufanya mazungumzo iwapo serikali
itakuwa tayari kuwaachia huru wanasiasa 11 wanaomuunga mkono ambao walikamatawa
wakati vurugu zilipotokea.
Machar aliyasema hayo baada ya serikali kusema ipo tayari kusitisha mapigano
makubaliano yaliyopokewa kwa mikono miwili na viongozi wa Afrika Mashariki mjini
Nairobi.
Mapigano yaliendelea siku ya ijumaa katika mji wa Makalal, katika jimbo la
Upper Nile.
Tayari askari zaidi wa Umoja wa Mataifa wa kuongeza nguvu wamekwishawasili
nchini Sudan Kusini.
No comments:
Post a Comment