TANGAZO


Saturday, December 28, 2013

Brotherhood wachoma Chuo Kikuu Misri

 


Chuo Kikuu cha al-Azhar kilichochomwa moto na waandamanaji

Wanafunzi ambao ni wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood lililopigwa marufuku nchini Misri wamepigana na polisi kwenye Chuo kikuu cha Al Azhar mjini Cairo.
Mwanafunzi mmoja ameuawa. Maafisa wa Usalama wanasema wanafunzi walijaribu kuwazuia wenzao wasifanye mtihani na baadae kuchoma moto kitivo cha biashara wakati polisi walipokuwa wakifyatua gasi ya machozi kuwatawanya.

 
Moto mwingine ulionekana katika kitivo cha kilimo. Polisi inasema watu 60 wanashikiliwa kutokana na tukio hilo.
Vurugu hizo zinakuja siku moja baada ya watu watano kuuawa nchini Misri kufuatia mapigano kati ya polisi na wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood.
Polisi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Al Azhar wamekuwa wakipambana mara kwa mara tangu rais wa zamani Mohammed Morsi alipoondolewa madarakani.
Watu watatu waanarifiwa kufa siku ya ijumaa wakati polisi walipokuwa wakipambana na wafuasi wa Muslim Brotherhood katika eneo la Minya ya Kusini na Nile Delta.
Mmoja ya waandamanaji amepigwa risasi na polisi wakati wanafunzi walipokuwa wakipigana na polisi katika Chuo Kikuu cha al-Azhar, maafisa wa wizara ya Afya wamesema'
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry wametoa wito kwa Waziri mwenzake wa mambo ya nje, kutilia umuhimu kuhusu matukio ya mara kwa mara ya polisi kukamata watu na kutaka kushirikishwaji wa kisiasa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani , Jen Psaki amesema.
Al - Azhar ni moja ya vyuo vikuu vyenye kufundisha elimu ya kiislamu ya madhehebu ya Sunni, ambacho kimekuwa na matuko ya kujirudia ya wanafunzi kupambana na polisi katika miezi ya hivi karibuni.
Mamlaka nchini Misri imekuwa ikiwasaka kundi la Muslim Brotherhood tangu mwezi julai, wakati aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi ambaye ni mfuasi wa kundi hilo alipoondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo.
Tayari kundi hilo limeshatangazwa kuwa ni kundi la kigaidi tangu jumatano.

No comments:

Post a Comment