Mali imetangaza mpango wa kumchunguza Rais wa zamani wa nchi
hiyo Amadou Toumani Toure kwa kosa la uhaini.
Ofisi ya Waziri Mkuu Oumar Tatam Ly imesema kwa njia televisheni kuwa
imewasilisha shauri hilo kwenye mahakama ya juu nchini humo.Serikali inamtuhumu Bwana Toure kwa kushindwa akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi wakati kundi la waislamu liliposhambulia eneo la kaskazini mwa nchi mwaka jana.
Bwana Toure alipinduliwa na jeshi mwezi April mwaka 2012 na kukimbilia uhamishoni nchini Senegal.
Mapinduzi hayo yalifanya Mali iangukie kwenye machafuko na kuruhusu muungano wa kundi la kikabila la Tuareg na wapiganaji wa kiislamu kuchukua eneo la kaskazini la jangwa la nchi hiyo.
Mapema mwaka huu kundi la wapiganji la kiislamu linaloungwa mkono na al-Qaeda liliondolewa katika miji mikubwa kwa msaada wa majeshi ya Ufaransa na ya Afrika ya Magharibi.
Siku ya Ijumaa msemaji wa serikali ya Mali, Mahamane Baby amesema Bwana Toure anachunguzwa kwa kuhusika kwake kwa kuvunja moyo askari kwa kuwawateua maafisa wa jeshi wasio na uwezo, ambao uwezo wao upo mashakani na kupewa nafasi kubwa jeshini.
Bwana Toure alijiuzulu rasmi mwezi April mwaka jana ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya askari kumrudishia madaraka.
Toure anasadikiwa kuishi uhamishoni nchini Senegal katika mji mkuu wa Dakar.
No comments:
Post a Comment