Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akichota maji kwenye kisima
alichokikabidhi kwa wakazi wa mtaa wa Kilimo, Kata ya Gongo la Mboto kama ishara
ya kukizindua rasmi, huku baadhi ya viongozi na wakazi wa mtaa huo
wakishuhudia.
Meya wa Ilala, Jerry Silaa akimkabidhi seti ya vifaa vya
michezo, mmoja kati ya manahodha wa timu zilizoshiriki ligi ya mpira wa miguu
katika kata ya Gongo la Mboto, ijulikanayo kama Jerry Super 8.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, ambaye pia
ni diwani wa kata ya Gongo la Mboto, akizindua rasmi kisima cha maji
kilichojengwa kwa ushirikiano wake na mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kilimo, Moshi Mwaluko.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto,
wakimsikiliza kwa makini Diwani wa kata yao, Meya wa Ilala, Jerry Silaa (hayupo pichani),
wakati akiwakabidhi vifaa vya michezo pamoja na kisima cha maji. (Picha zote na mdau wetu)
No comments:
Post a Comment