Pages

Saturday, September 22, 2012

Yanga yaonesha makali yake, yaipiga JKT Ruvu mabao 4-1, Uwanja wa Taifa

Wahezaji wa timu za Yanga na JKT Ruvu wakiingia uwanjani tayari kwa mpambano wao wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam leo jioni. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Wachezaji wa timu za Yanga na JKT Ruvu, wakisalimiana tayari kwa mchezo wao, uwanjani hapo leo jioni.
 
 Kikosi cha timu ya Yanga, kilichojitupa uwanja wa Taifa kupambana na JKT Ruvu leo jioni katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
 Kikosi cha timu ya JKT Ruvu, kilichopambana na Yanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

 Mchezaji wa Yanga, Didier Kavumbagu, akimtoka Damas Makwaya wa JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Yanga imeirarua JKT Ruvu mabao 4-1.

 Hamis Kiiza wa Yanga, akipita mbele ya golikipa wa JKT Ruvu, Said Mohamed, aliyeutokea mpira na kuudaka.

 Ally Khan wa JKT Ruvu, akimtoka Didier Kavumbagu wa Yanga katika mchezo huo.

Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo kati ya timu hizo, na Yanga kuibuka washindi wa mchezo huo, ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni na Yanga kufanikiwa kuifunga timu hiyo.

Mashabiki wa Yanga wakifuatilia kwa makini mchezo kati ya timu hizo na Yanga kuibuka washindi wa mchezo huo, ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
 
Mchezaji Simon Msuva wa Yanga, akipiga shuti kuelekea langoni kwa JKT Ruvu katika mchezo huo leo jioni, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 Wachezaji Jerryson Tegete wa Yanga (katikati) na Charles Timoth wa JKT Ruvu wakisigana kuwania mpira katika mchezo huo.

Wachezaji Hamis Kiiza wa Yanga (kushoto) na Damas Makwaya wa JKT Ruvu wakipambana kwenye kibendera kuwania mpira katika mchezo huo.

Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo na JKT Ruvu, uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga kuibuka washindi wa mchezo kwa kuifunga timu hiyo mabao 4-1.


Hadi mwisho wa mchezo huo, ubao wa matokeo ulikuwa ukionesha Yanga mabao 4 na JKT Ruvu bao 1.

No comments:

Post a Comment