Pages

Sunday, September 23, 2012

Maonesho ya usiku wa mitindo, Mbalamwezi Beach jijini Dar es Salaam

 

Mtangazaji katika maonesho hayo, Ireene Tilya ambaye ni Mtangazaji wa Toneradio, akiwa anaendelea na kazi yake hiyo.

Mmoja wa wanamitindo  mbalimbali, akipita katika hadhira hiyo.

Mmoja wa waoneshaji mitindo, akipita kwenye jukwaa.

 

Muonesha mitindo akipozi katika kuonesha vazi alilolivaa.

Umeniona, hiyo ndiyo kauli inayoashiria kutoka kwa muoneshaji mitindo huyo.

Wadau mbalimbali waliofika kutazama mashindano hayo, wakiangaza huku na kule.

Wanamitindo wakifuatilia waoneshaji mitindo ya mavazi yao, wakati wa maonesho hayo.

Akina kaka nao walipendezesha vilivyo tukio hilo la maonesho ya Mavazi

Mmoja wa waonesha mitindo, akiwa kazini.

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Vyombo vya habari wa Kampuni ya Mult-Media, Victor Luvena (kushoto), akiwa na Afisa Masoko wa Tone, Harold Mwakasala wakati wa maonyesho ya mitindo ya mavazi yaliyofanyika Septemba 22, mwaka huu, Mbalamwezi Beach.

Wabunifu wa mavazi katika usiku wa mitindo uliofanyika Mbalamwezi beach walikuwa ni Diana Magese, Mitindonite iliwakilishwa na Ally, Amin, Wancy na Matrida, Bambo collection, Renee, Cocoriko, William Johnson, Veronica Ruhenzi-VS collection, Dorcas, Subira, Salim Ally, na Wavisa Collection.

Wengine ni Onfe collection, Baby Jullieth Collection na Hamidi Abdul collection.

Maonyesho ya mitindo ya mavazi, yameandaliwa na Mitindonite Afrika na kudhaminiwa na Darling, Equity Bank, Tone Mult-Media Company Limted ambao ni wamiliki wa Tone radio, Blogs za mikoa na Thisday Magazine, Secret Lengerie wauzaji wa nguo za ndani za wanawake, Amaya Beauty Solon & Spa, Better service, small axe, Qice photo sport, Real Burger, Fashion News, Pekuatanzania na Mdee Trans.

No comments:

Post a Comment