v WAKILI GABLIEL MALATA APATA KIBANO CHA KISHERIA TOKA KWA SHAHIDI JORAN BASHANGE, NAIBU KATIBU MKUU NA KUSHINDWA KUFANYA [CROSS EXAMINATION].
v JAJI AMJIBU MALATA KUWA ANAANDIKA MAMBO YANAYOHUSIANA NA SHAURI TU [RELEVANT QUESTIONS].
v MAHAKAMA KUU YAKATAA MAOMBI YA MALATA KUTAKA GHARAMA ZILIPWE KATIKA SHAURI NA. 28/2017.
v WAKILI MALATA AJARIBU KUTETEA SAINI FEKI YA LIPUMBA KWA KUDAI KUWA KABADILISHA SAINI YA MWANZO NA SASA ANATUMIA NYINGINE.
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
TAARIFA KWA UMMA
Dated: 08 JUNE, 2018
MBELE YA MAHAKAMA KUU MHE JAJI DYANSOBERA , amekataa maombi ya Wakili Gabriel Malata ya kutaka kulipwa Gharama katika shauri Namba 28/2017 lihusulo maombi ya Zuio ya Ruzuku ambalo lilifunguliwa mwanzo kabla ya Shauri Namba 80/2017. Shauri hili lilikuja leo kusikilizwa na Hoja zilikuwa kama ifuatavyo;
Wakili Juma Nassoro: Mhe Jaji tunaomba shauri hili liondolewe mbele ya Mahakama yako tukufu kwa kuwa Mahakama yako ishafanya maamuzi katika maombi kama haya yaliyowasilishwa katika Mahakama hii.
Malata: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi juu ya maombi hayo. Isipokuwa tunaomba muombaji alipe Gharama za shauri hili. [Applicant ni The Registered trustees of The Civic United Front-CUF-Chama Cha Wananchi]. Akijenga hoja zake ameeleza Mahakama kuwa Serikali imeingia gharama kuandaa kulishughulikia shauri hili. Pili, wameomba wamefungua shauri juu ya shauri na hivyo ni mchezo wa kuisumbua Mahakama. Tatu, tumefanya maandalizi, tumejiandaa na kuhudhuria mahakamani mara kadhaa. Nne fedha zinazoombwa si za Malata ni za serikali ili kuhudumia maeneo mengine, kwa mujibu wa Kifungu cha 13 cha Government Proceedings Act,
Wakili Juma Nassoro: katika kujibu hoja hizo ameileza Mahakama kuwa;
1. Mpaka maombi ya kuliondoa shauri hilo yanawasilishwa Mahakamani hakuna Pingamizi lolote lililowekwa na Wajibu Maombi [Respondents] juu ya uwepo wa shauri hilo.
2. Shauri hili limetokana na shauri la msingi namba 21/2017 ambalo mahakama imeliondoa mahakamani [Stricken Out].
3. Shauri namba 80/2017 linatokana na Shauri Namba 68/2017 hivyo ni vitu viwili tofauti.
4. Kutokana na Amri ya mwisho kutolewa na Mahakama hii juu ya shauri namba 80/2017 haina haja tena ya uwepo wa shauri namba 28/2017
5. Hatuombi shauri hili liondolewe kwa sababu tumeshindwa kuliendesha. Hapana . kwa sababu mahakama ishatoa maamuzi katika maombi yanayofanana na hayo.
6. Hoja kuhusu gharama. Malata ni mtumishi wa serikali atalipwa mshahara hata asipoweza kuhudhuria mahakamani tofauti na sisi mawakili wa kujitegemea.
7. Hoja ya gharama si mara zote hutolewa bali inategemea na mazingira ya shauri husika.
MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU:
Baada ya kusikiliza hoja hizo Mahakama iliekeza kuwa;
Suala la kulipa gharama linatokana na busara/mamlaka ya Mahakama [Court Discretion] katika mazingira ya shauri hili. Mahakama hii imemzuia Respondent namba moja Msajili wa Vyama asitoe Ruzuku ya CUF. Kumtaka Applicant alipe gharama wakati sote tunajua kuwa vyanzo vya fedha kwa Taasisi hii ni Ruzuku ni Mahakama kujichanganya. Hivyo Mahakama imeliondoa shauri hilo bila Gharama.
KUHUSU SHAURI NAMBA 13/2017 ALLY SALEH DHIDI YA RITA, LIPUMBA NA WENZAKE:
Shahidi wa pili katika shauri namba 13/2017 Mhe. Joran Bashange [Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Mkurugenzi Wa Fedha Na Katibu Wa Bodi ya Wadhamini ya CUF] ameendelea kufanyiwa [cross examination] na Wakili Gabriel Malata. Mhe Bashange amembana vilivyo Malata kwa kujibu maswali kwa ufasaha na kumfilisi Malata hata asijue nini cha kuuliza. Katika vituko vilivyotokea leo ilifika wakati ambapo Jaji alimuachia Malata kupwaga na maswali yasiyowiana na hoja iliyopo mezani na alipogundua hivvyo ikabidi akae chini. Mahakama ilimjibu kuwa inarekodi masuala [Relevant Questions].
WAKILI MSOMI WAKILI DAIMU HALFANI alilazimika kuingilia kati na kumtaka Wakili Malata kujielekeza katika masuali ya msingi na kuacha kupoteza muda.[ you must behave properly as Principal State Attorney and not otherwise] alisema. Vilevile WAKILI MSOMI LOVENESS DENIS [KUTOKA CHAMBER YA MHE MPOKI]alimuomba Malata kujielekeza katika maswali ya msingi. Hii ilitokana na mambo ya kipuuzi kuwa mengi na kubishana na muongozo wa Mahakama wa kuuliza Closed Question and Not Open Questions ambayo huzua majibizano na shahidi. Jibu la shahidi kwa swali na Wakili anayefanya Cross exam…linapaswa kuwa ndio au hapana.
Vituko vingine ni pale Malata kudai kuwa Lipumba kabadili saini yake ya awali na sasa anatumia saini mpya ambayo Mhe Bashange ameieleza Mahakama kuwa saini inayoelezwa kuwa ya Lipumba siyo na kwamba IMEGHUSHIWA. Wakili Malata anajaribu kutaka kutetea saini iliyoghushiwa kuwa ni saini halali ya Lipumba. Leo malata amekamilisha kumuhoji shahidi namba mbili na sasa itafuata zamu ya mawakili wengine.
Kutokana na wakili Malata kushindwa kujielekeza vyema katika maswali yake kwa Shahidi imekuwa ni vigumu hata kunukuu maswali hayo na majibu yake kutokana na ubishani na vikwazo alivyokutana navyo kwa Shahidi Bashange katika kujibu maswali yake.
RATIBA YA MASHAURI JUNE/JULY, 2018;
1. Shauri La RITA Litaendelea Tarehe 5 July
2. Wabunge Viti Maalumu Tarehe 20 Na 22 June
3. Uchaguzi Feki Wa Lipumba Tarehe 29 June.
THE NEW, STRONG, AND VIBRANT CUF IS COMING BACK SOON.
HAKI SAWA KWA WOTE
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa Leo Tarehe 08/6//2018 na Kurugenzi ya Habari CUF-Taifa
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI-NMHUMU
Tigo-0715 062 577, Voda -0767 062 577
No comments:
Post a Comment