TANGAZO


Sunday, May 27, 2018

ZIARA YA NAIBU WAZIRI DKT. NDUGULILE UWANJA WA NDEGE WA J.K NYERERE

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akihoji ufanisi wa utendaji kazi wa moja ya mashine ya kupima na kutambua dalili za mgonjwa mwenye EBOLA zilizopo Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere Dkt. George Ndaki wakati alipofanya ziara katika Uwanja huo ili kujiridhisha na utendaji na ufanisi wa mitambo ya kutambua dalili za mgonjwa mwenye EBOLA.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiendelea na Ziara katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere jijini Dar es salaam akiongozana na mwenyeji wake Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja huo.  
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine akitoa maelekezo kwa Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere Dkt. George Ndaki pindi alipofanya ziara jana katika uwanja huo. 

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika eneo la kupokelea mizigo wakati akiendelea na ziara yake, kulia kwake ni Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere Dkt. George Ndaki kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa huduma za kinga Dkt. Khalid Massa.

Na WAMJW-DSM
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imeridhika na maandalizi ya mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko ukiwemo ugonjwa wa Ebola katika mipaka yote na viwanja vya ndege nchini

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere 

Dkt.Ndugulile amesema amefika hapo ili kuangalia hali ya maandalizi na ufungaji wa mashine za kisasa za utambuzi wa ugonjwa wa Ebola endapo itatokea mtu mwenye ugonjwa huo

Aidha, alisema wizara imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa nchini na kuweka mfumo wa kubaini watu wanaoingia kwa kubaini hali ya joto linaloongezeka kwa  mgeni anayeingia na kufanyiwa uchunguzi zaidi.

"tumeweka mfumo wa kuwafuatilia wale ambao watakua wamebainika na joto zaidi mahali watakapofikia na mawasiliano yao ili kujua hali zao na endapo atapata mabadiliko"

Naibu huyo aliongeza kuwa wamewafanyia mazoezi ya kutosha kwa watoa huduma wa mipakani na viwanja vya ndege na pia kuwapatia elimu jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Dkt.Ndugulile ameendekea kusisitiza na kuwatia hofu wananchi kwamba hadi sasa hakuna mtu alobainika kuwa na ugonjwa wa Ebola na hali ya mipaka ya Tanzania ni Salama

No comments:

Post a Comment