TANGAZO


Friday, April 13, 2018

DRC yasusia mkutano wa Umoja wa mataifa Geneva ulioandaliwa kuisaidia nchi hiyo

Rais Joseph Kabila

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionRais Joseph Kabila
Umoja wa mataifa hii leo unafanya mkutano maalum mjini Geneva Uswizi kuchangisha fedha za kukabiliana na janga la kibinaadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Mashirika ya misaada yanasema zaidi ya watu milioni 5 wamelazimika kuyatoroka makaazi yao kwasababu ya mapigano katika sehemu tofauti ya nchi hiyo kubwa.
Lakini serikali ya DRC imekataa kuhudhuria mkutano huo wa ufadhili ikisema kwamba hali inafanywa kuwa mbaya wakati ni kinyume cha hicho.
mama na watoto wakimbizi DRCHaki miliki ya pichaNRC/CHRISTIAN JEPSEN
Mkutano huo umedhamiriwa kuchangisha dola bilioni 1.7 kupunguza uzito wa inachotajwa na Umoja wamataifa kuwa ni janga kubwa la binaadamu nchini Congo.
Mpaka sasa serikali ya DRC haijajibu mualiko wa Umoja wa mataifa ikisema taasisi hiyo kuu imetilia chumvi hali halisi nchini na ukubwa wa tatizo lililopo.
Mashirika ya misaada yanasema watu milioni tano wamelazimika kuyatoroka makaazi yao kutokana na ghasia, mapigano, njaa na ukosefu wa utulivu na kwamba maelfu ya raia wa Congo wamelazimika kutafuta hifadhi magharibi mwa Uganda.
Wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu ndani ya DRC wamezusha wasiwasi kutokana na hatua hiyo ya serikali kususia mkutano huo mkuu mjini Geneva.
Kumeshuhudiwa ghasia na maandamano nchini kumshinikiza rais Joseph Kabila aondoke madarakani
Image captionKumeshuhudiwa ghasia na maandamano nchini kumshinikiza rais Joseph Kabila aondoke madarakani
Wasiwasi wa aina hiyo pia umetolewa na baadhi ya raia wanoasema kwamba wataendelea kuteseka bila ya msaada wa kimataifa.
Je kuna hasara gani wa kwa serikali hiyo kukataa kuhudhuria mkutano wa Geneva?
Mashirika ya misaada yanasema DRC inateseka katika janga kubwa lenye uzito la kibinaadamu lililosahaulika kwa muda mrefu.
Kuna watu milioni 13 wanaohitaji usaidizi: miongoni mwao watoto milioni 2 wanaugua utapia mlo mbaya, na watu milioni 4.5 wamepoteza makaazi yao.
Lakini tathmini hii ya mashirika ya misaada imeiudhi serikali ya DRC.
Inatizama kiwango cha daraja la tatu kilichowekwa cha hali ya janga hilo kuwa kama tusi.
Mashirika ya misaada yanasema watu milioni 13 wanahitaji usaidizi: miongoni mwao watoto milioni 2Haki miliki ya pichaNRC/CHRISTIAN JEPSEN
Image captionMashirika ya misaada yanasema watu milioni 13 wanahitaji usaidizi: miongoni mwao watoto milioni 2
Na ndio sababu ikachukua hatua hii ambayo haikutarajiwa ya kususia mkutano wa Geneva.
Maafisa hatahivyo wa Umoja wamataifa wanatumai kwamba wanadiplomasia wa Congo watabadili uamuzi wao na wahudhurie mkutano huo leo.
Ni wazi kwamba mkutano wenyewe utaendelea licha ya chochote kile kitachotokea, wanaharakati wanasema maisha ya mamilioni ya watu yamo hatarini.

No comments:

Post a Comment