
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kinga Amos Maziku akitoa mafunzo ya huduma bora kwa wateja kwa wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na JKCI)
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kinga Amos Maziku (hayupo pichani) wakati akitoa mafunzo ya utoaji wa huduma bora kwa wateja yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kinga Amos Maziku (hayupo pichani) wakati akitoa mafunzo ya utoaji wa huduma bora kwa wateja yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kinga Amos Maziku (hayupo pichani) wakati akitoa mafunzo ya utoaji wa huduma bora kwa wateja yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi alizungumza na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kinga Amos Maziku mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya utoaji wa huduma bora kwa wateja yaliyotolea leo kwa wafanyakazi wa JKCI.
Mkufunzi wa masuala ya fedha na maisha bora kutoka Taasisi ya Kinga akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kuongeza kipato nje ya mshahara kwa kujihususha na ujasiriamali wakati wa mafunzo ya utoaji wa huduma bora kwa wateja yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
07/03/2018
WAFANYAKAZI wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wameshauriwa kuendelea kuwahudumia wagonjwa kwa usawa bila ya kuonyesha upendeleo kutokana na hali zao za maisha.
Ushauri huo umetolewa leo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kinga Amos Maziku wakati akitoa mafunzo ya huduma bora kwa wateja yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete .
Maziku alisema iwapo wagonjwa wote watahudumiwa kwa usawa bila ya kuwabagua kutokana na hali zao za maisha kutawaongezea watoa huduma kujijenga zaidi katika utendaji kazi na hivyo kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
“Ipende kazi yako na kuwathamini wagonjwa unaowahudumia kwa kuhakikisha wanapata huduma kwa wakati na kuwasikiliza matatizo yao”.
“Unapomuhudumia mgonjwa jitahidi kumzoea, muhudumie ukiwa unatabasamu, muite kwa jina lake na uwe nadhifu na msafi wakati wote kwani mfanyakazi unaiwakilisha Taasisi yako pia muwe wabunifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea badilika kutokana na mazingira yaliyopo”, alisisitiza.
Akifundisha jinsi ya kuongeza kipato nje ya mshahara Alphonse Chilato ambaye ni Mkufunzi wa masuala ya fedha na maisha bora kutoka Taasisi ya Kinga aliwasisitiza wafanyakazi hao kutumia vizuri muda wao wa ziada baada ya kutoka kazini ikiwa ni pamoja na kujifunza mambo mapya katika maisha yao.
Chilato alisema, “Hivi sasa simu za mkononi zina kila kitu tumieni simu zenu vizuri katika kujifunza teknolojia. Unaweza kutumia simu yako kuzalisha fedha kwa kufanya ujasiriamali lengo likiwa ni kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi aliwashukuru waandaaji wa mafunzo hayo ambayo yatasaidia kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wateja wa Taasisi ambao wengi wao ni wagonjwa.
Prof. Janabi alisema, “Wafanyakazi wa Taasisi hii wamekuwa wakitoa huduma bora kwa wateja wetu, nitahakikisha huduma hii inaendelea kuwa bora zaidi ili Hospitali yetu iwe ya mfano wa kuigwa hapa nchini na nje ya Nchi.
Mafunzo hayo ya utoaji wa huduma kwa wateja ni moja ya mikakati ya Taasisi hiyo ya kuhakikisha wafanyakazi wake wanatoa huduma bora ya matibabu ya moyo kwa wagonjwa wanaowahudumia.



No comments:
Post a Comment