Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayesimamia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka akieleza mpango wa Wizara katika kusimamia Sekta ya Maendeleo ya Jamii kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati akifungua Kikao cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro Kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George.Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George akieleza dhumuni la kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro.
Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Abel Palala akiwasilisha mada kuhusu Mtaala wa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Stashahada katika kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii waliokutana kujadili Mitaala pendekezi ya fani ya Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa TAFOLI Mjini Morogoro. Mhadhiri wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Bw. Simon Kilasala akitoa taarifa ya utafiti wa Soko la ajira kwa wataalam wa Maendeleo ya Jamiki wakati wa kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wanaokutana kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa TAFOLI Mjini Morogoro.
Mkufunzi Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba Bw. Kidubya Kulamiwa akiwasilisha mada kuhusu Mtaala wa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Astashahada katika kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha siku moja cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii waliokutana kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro.
Mkufunzi Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare mkoani Mara Bw. Anicet Rwezaula akiwasilisha mada kuhusu Mtaala wa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Cheti cha Msingi katika kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii waliokutana kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro.
Baadhi ya wadau na wataalamu wa Maendeleo ya Jamii wakijadiliana katika makundi ili kutoa maoni na kuboresha Rasimu ya Mitaala ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao kilicho wakutanisha Mjini Morogoro hivi karibuni.
Baadhi ya wadau na wataalamu wa Maendeleo ya Jamii wakijadiliana katika makundi ili kutoa maoni na kuboresha Rasimu ya Mitaala ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao kilicho wakutanisha Mjini Morogoro hivi karibuni.
Na Mwandishi Wetu Morogoro
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) imeahidi kuimarisha taaluma ya Maendeleo ya Jamii ili iweze kuongeza tija katika jamii.
Hayo yamesemwa mjini Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka wakati wa kikao cha wadau waliokutana kujadili rasimu ya mitaala na kupata maoni yatakayowezesha kuboresha mitaala ya vyuo hivyo.
Bi. Neema amesema kuwa Wizara itafuatilia kwa karibu utoaji mafunzo ya fani ya Maendeleo ya Jamii kwa vyuo vyake inavyovisimamia na pia kushirikiana na Mamlaka nyingine katika kufuatilia utoaji wa mafunzo hayo kwa Vyuo visivyosimamiwa na Wizara.
“Kikao cha wadau cha kupitia mitaala ya vyuo vya maendeleo ya jamii kinajenga uwezo wa Wizara katika kuhakikisha usimamizi wa vyuo hivi unazingatia Kanuni na taratibu za Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) jukumu ambalo Wizara imekuwa ikilitekeleza kila inapohitajika” alisisitiza Bi Neema.
Akizungumza katika mkutano huo Kaimu Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George suala la kuwa na mkutano wa wadau kupitia rasimu ya mitaala ya vyuo vya Maendeleo ya Jamii ni hitaji la muhimu ili kupta maoni ya takayosaidia kkuboresha mada, mahudhui, mbinu, stadi za kufundishia na kujifunzia na maarifa.
Dkt. Bakari aliongeza kuwa awali Wizara iliandaa utafiti wa mahitaji, kubaini majukumu na wajibu wa wataalam wa maendeleo ya jamii, na hatimaye kuweza kuandaa rasimu ya awali ya mitaala ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kuimarisha umahiri wa Vyuo vya Maendeleo ya jamii, weledi wa wataalam wa maaendeleo ya jamii na kutoa mchango katika kufikia maendeleo jumuishi.
“Wizara inaandaa mitaala ya vyuo vya maendeleo ya jamii ili kujenga umahiri wa vyuo na kuchangia ujenzi wa Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati” alisema Dkt. Bakari.
Naye Mhadhiri wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Bw. Simon Kilasala amesema kuwa utafiti uliofanyika kuhusu mitaala ya vyuo vya maendeleo ya jamii umebainisha kuwa wahitimu wengi kutoka katika vyuo hivyo bado wanahitaji stadi zaidi katika kuongeza mbinu na umahiri ziada wa kuweza kujiajiri na kutengeneza ajira mpya.
“Utafiti huu utasaidiakuboresha Mitaala ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kutokana na mahitaji ya soko la ajira kwa wataalm wa Maendeleo ya Jamii nchini na nje ya nchi” alisisitiza Bw. Kilasala
No comments:
Post a Comment