TANGAZO


Saturday, March 17, 2018

Jacob Zuma akabiliwa na mashtaka ya rushwa

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepatikana na mashtaka 16 ya rushwa inayohusishwa na mamilioni ya dola yaliotumika katika mpango wa silaha.
Mashtaka hayo ambayo bwana Zuma amekataa kuhusika yanajumuisha udanganyifu aliofanya ili kujipatia fedha na utakatishaji wa fedha.
Bwana Zuma mwenye umri wa miaka 75,chama chake cha ANC kilimlazimishaa kuachia madaraka yake mwezi uliopita.
Zuma alipigiwa kura ya kutoamaniwa mara ya tisa katika bunge kabla hajaachia ngazi.
Mwendesha mashtaka mkuu Shaun Abraham amesema anaamini kuwa kuna sababu ya kuwa na mtazamo chanya juu ya hukumu ya kesi hii.
Msambazaji wa silaha kutoka Ufaransa Thales yeye pia atakabaliwa na mashtaka .Taarifa kutoka AFP zinasema Thales amekataa kuongea chochote kuhusu suala hilo.
Bwana Zuma anatuhumiwa kutaka rushwa kutoka kwa Thales kwa nia ya kuboresha maisha yake ya kifahari.Mshauri wake wa fedha wakati huo alikutwa na hatia ya kuomba rushwa hizo mwaka 2005 na bwana Zuma alimfukuza kazi yake ya usaidizi wa rais.
Mashtaka ya awali dhidi ya bwana Zuma yalikuwa yameondolewa muda mfupi kabla ya kuwa rais mwaka 2009.
Kwa sasa anakabiliana na shitaka moja la kusababisha ghasia,mashtaka mawili ya rushwa,shtaka moja la rushwa na mashtaka 12 ya udanganyifu.

No comments:

Post a Comment