TANGAZO


Friday, March 16, 2018

Hoja tatu kutoka kwa hotuba ya Mugabe

Robert Mugabe

Haki miliki ya pichaEPA
Chama cha National Patriotic Front, NPF, kilichoundwa na waliokuwa mawaziri wa Zanu PF kimemtangaza Rais wake.
Chama hicho kipya kimetangaza kuwa Brigedia mstaafu Ambrose Mutinhiri atakuwa Rais wake, hatua ambayo inaelezwa kuungwa mkono na Robert Mugabe.
Ijumaa juma lililopita, Mutinhiri alijiuzulu ubunge na ndani ya Zanu PF, akionyesha kutounga mkono kuondolewa kwa Mugabe madarakani.
Mkutano wa Mugabe wa kwanza na waandishi wa habari tangu aondoke madarakani inasemekana uliandaliwa na chama cha NPF ambacho kina matumaini ya kumuondoa
Mnangagwa kwenye kinyang'anyiro cha mwezi Agosti.
Kwa miezi kadhaa sasa imekuwa ikidhaniwa kuwa huenda Mugabe atarejea tena kwenye ulingo wa siasa dhidi ya chama chake cha zamani.
Lakini ni mambo yapi haswa aliyoyasema Mugabe kwenye hotuba yake?
Aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert MugabeHaki miliki ya pichaZNBC
Image captionAliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe

''Sikudhani kama angeweza kunigeuka'' Alisema Mugabe

Mugabe amesema kuwa Mnangagwa asingeweza kumuondoa madarakani kwani ni yeye ndiye aliyemuweka serikalini, alimsaidia alipokuwa gerezani, na hakuwaza kuwa siku moja Mnangagwa angemtoa madarakani.
Mnangagwa anajulikana kama "mamba"
•Alipata mafunzo ya jeshi nchini China na Misri
•Alisaidia kuongoza kupigania uhuru nchi ya Zimbabwe miaka ya 70
•Alikuwa jasusi wa nchi wakati wa mgogoro wa ndani kwa ndani ambapo maelfu wa wananchi waliuwawa.
•Anajulikana kama kiungo baina ya jeshi, idara ya ujasusi na chama cha Zanu- PF
Military officers pins insignia on President Emmerson MnangagwaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMugabe anaona kuingia Mnangagwa madarkani ni usaliti
''Yalikuwa mapinduzi ya kijeshiJeshi lilitumika kutekeleza azima hiyo''
Aliyekua Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anavunja ukimya kwa mara ya kwanza tangu aondolewe Madarakani, amesema kuwa amekua muhanga wa mapinduzi ya kijeshi.
Akiongea na televisheni ya SABC ya Afrika kusini Mugabe amesema kuwa Rais wa sasa Emerson Mnangagwa asingeweza kuingia madarakani bila kutumika kwa jeshi.
Mugabe amekemea mbinu zilizotumika kumuondoa madarakani.
Amesema alikua tayari kufanya mazungumzo na Rais wa sasa Emerson Mnangagwa na angehakikisha mabadiliko ya madaraka ya uhalali na si yale ya kulazimishwa.
Mugabe alisema kuwa yuko tayari kwa ajili ya Mazugumzo na Mnangagwa ili kulinda katiba yao.
Zimbabwe's Army commander General Constantine Chiwenga (L) chats with commander of the Zimbabwe National Army, Lieutenant-General Phillip Valerio Sibanda, during the country's 28th year of independence celebration in Harare on April 18, 2008.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMkuu wa majeshi ya Zimbabwe Constantino Chiwenga (kushoto) ni rafiki wa karibu wa Mnangagwa

''Hatuna budi kuondosha aibu hii''

Mugabe ametumia nafasi yake kwa kiasi kikubwa kwenye mazungumzo na waandishi wa habari tangu alipotolewa madarakani, akieleza namna ambavyo aliondolewa kwa ''mapinduzi'' yaliyokuwa yamekiuka sheria.
Alisisitiza kwa kauli yake ''tuondoshe aibu hii'' akirejea namna alivyoondolewa madarakani na kama watu watamtilia maanani tena baada ya yaliyotokea.
Ni rahisi, na yenye kushawishi, kuhitimisha kuwa Zimbabwe inaendelea na maisha, lakini madai ya Mugabe kuwa Mnangagwa ni mtu mbaya, asiyestahili, mtu mwenye kinyongo yameonekana kupuuzwa na taifa hilo na hata jamii ya kimataifa, ambayo inamuunga mkono Rais mpya.
Soma pia:

No comments:

Post a Comment