TANGAZO


Thursday, March 15, 2018

Antonio Conte asema Chelsea kuchapwa 3-0 na Barcelona UEFA haikuwa haki

Antonio Conte greets Lionel Messi at the final whistle.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLionel Messi alifunga bao lake la 100 katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kusaidia kuwalaza Chelsea 3-0 uwanjani Nou Camp
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema alihisi kwamba kichapo cha 3-0 ambacho klabu yake ilipokezwa katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano "hakikuwa cha haki".
Lionel Messi alifunga mabao mawili naye Ousmane Dembele akafunga moja - bao lake la kwanza akichezea Barca - na kuwasaidia miamba hao wa Uhispania kuondoka na ushindi wa jumla wa 4-1.
Mechi ya kwanza uwanjani Stamford Bridge ilikuwa imemalizika 1-1.
Matokeo hayo yaliwaondoa Chelsea kutoka kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu na msimu ujao wanakabiliwa na kibarua cha kufuzu kutokana na ushindani mkali kwenye nafasi nne za kwanza Ligi ya Premia.
"Hatuna majuto," alisema Conte.
"Ukiitazama mechi hiyo, utaona kwamba matokeo hayo hayakuwa ya haki."
Conte alikiri kwamba Messi - aliyefunga pia bao la Barca mechi ya kwanza Stamford Bridge - ndiye aliyekuwa mwamuzi wa nani mbabe kati ya timu hizo mbili.
Bao la pili la mshambuliaji huyo wa Argentina uwanjani Nou Camp lilifikisha 100, idadi ya mabao ambayo ameyafunga Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Antonio Conte and Lionel MessiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionLionel Messi akipongezwa na meneja wa Chelsea Antonio Conte baada ya mechi Jumatano
Mpinzani wake mkuu kutoka Real Madrid Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi akiwa na mabao 117.
Hata hivyo, Messi amefikisha idadi hiyo akiwa amecheza mechi 14 chini ya alizocheza Ronaldo ndipo afikishe mabao hayo.
"Tunazungumzia mchezaji bora zaidi duniani," alisema Conte.
"Huwa anafunga mabao 60 kila msimu - ni mchezaji mzuri ajabu. Barcelona walikuwa na ufasaha sana wakishambulia."
Klabu nane zilizofuzu..
Klabu zilizofika robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu ni: Barcelona, Bayern Munich, Juventus, Liverpool, Manchester City, Real Madrid, Roma na Sevilla.
Droo itafanyika Nyon, Uswizi saa 11:00 GMT Ijumaa
Chelsea waliongoza kwa dakika 13 mechi ya kwanza na waligonga mwamba na mlingoti wa lango mara nne katika mechi zote mbili.
N'Golo Kante na Marcos Alonso wote walikaribia kufunga uwanjani Nou Camp, naye Antonio Rudiger alipiga mpira wa kichwa ambao uligonga mwamba wa goli dakika za mwisho.
Blues walinyimwa ombi lao la kutaka penalti Alonso alipoanguka eneo la hatari baada ya kukabiliwa na Gerard Pique.
"Hatukustahili kushindwa 3-0," alisema Conte.
"Tulikosa bahati kiasi.
"Tafikiri tulitengeneza naafsi nyingi lakini hatukuzitumia.
"NI lazima nijivunie sana wachezaji wangu - walijitolea kabisa na ni lazima tuendelee hivi, nia hii ya kupambana na kupigana vita pamoja uwanjani."
Chelsea playersHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWachezaji wa Chelsea waliotamauka wakiondoka uwanjani baada ya kushindwa Nou Camp
Courtois hatarajia kombora la Messi
Mlindalango wa Chelsea Thibaut Courtois aliambia BT Sport kwamba anaamini makosa ya wachezaji binafsi yaliigharimu timu hiyo.
"Sifikiri kwamba tulifaa kuondolewa, lakini makosa ya wachezaji binafsi yalitugharimu ushindi mechi zote mbili.
"Bao la kwanza ... Sikutarajia Lionel Messi angetoa kombora kutokana na pahali ambapo alikuwa na nilichelewa kufunga mwanya kati ya miguu yangu. Hilo lilikuwa kosa langu.
"Pahali dhaifu zaidi huwa ni katikati ya miguu ya golikipa. Inaudhi. Siwezi kujificha ndani (ya lango), ni lazima niwe kama mwanamume na kutokea."
Antonio ConteHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionAntonio Conte atakutana na Leicester Jumapili kupigania nafasi ya kufuzu kwa nusufainali katika Kombe la FA
Winga wa Chelsea Marcos Alonso aliambia BT Sport kwamba walifahamu kwamba Barca wana wachezaji wazuri sana.
"Na hatuwezi kuwapa nafasi, hata mita moja, kwa sababu wanaweza kuunda nafasi na kufunga."
Amesema sasa ni lazima warudi kujiboresha zaidi, kufanya mazoezi na "kujiboresha".
Lionel Messi celebrates scoring for Barcelona against Chelsea in the Champions LeagueHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLionel Messi akisherehekea baada ya kuwafunga Chelsea
Wafungaji mabao bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
WachezajiMechiMabao
Cristiano Ronaldo148117
Lionel Messi123100
Raul14271
Ruud van Nistlerooy7356
Karim Benzema10053
Thierry Henry11250
Zlatan Ibrahimovic12048
Andriy Shevchenko10048
Filippo Inzaghi8146
Robert Lewandowski6845

No comments:

Post a Comment