TANGAZO


Saturday, February 17, 2018

WANANCHI JIMBO LA SIHA WAPIGA KURA KWA AMANI

Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Giveness Aswile akizungumza jambo kwenye kitu cha kupigia kura cha Dula la Ushiriki 1 wakati akikagua upigaji kura. Kulia kwake ni Mjumbe wa NEC Jaji Mst. Mary Longway.(Picha zote na Hussein Makame, NEC)
Msimamizi wa Kituo cha Kupigia Kura cha Ofisi ya Kijiji Sanya Hoyee akipokea kadi ya kupigia kura ya mpiga kura aliyejitambulisha kwa jina la Mariyelo aliyeambatana na msaidizi wake kupiga kura.
Mjumbe wa NEC Jaji Mst. Mary Longway akisalimiana na Bibi Mariyelo baada ya mpiga kura huyo kupiga kura.  
Mmoja ya wapiga kura akipiga kurakwenye kituuo cha Ofisi ya Kijiji ya Magadini 01, kumchagua Diwani wa Kata ya Gararagua katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro. 
Baadhi ya wapiga kura wakiwa wamejipanga mstari nje ya kituo cha Cluster Sanya Juu B wakisubiri kupiga kura. 
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Giveness Aswile (kulia) akimuangalia mpiga kura akitimiza haki yake ya kumchagua Mbunge wa Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro. 

Mwandishi wetu
17/2/2018-Siha, Kilimanjaro
UPIGAJI kura  kwa katika Uchagua Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Siha na wa Madiwani katika Kata 3 za Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro unaendelea vizuri.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  ikiongozwa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway na Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bi Giveness Aswile, mapema leo ilitembelea vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kufuatilia upigaji kura.

Tume ilitembelea vituo vya kupigia kura vilivyoko katika Kata ya Mabanzini vya Shule ya Msingi Kilingi, Ofisi ya Kijiji Sanya Hoyee, Kata ya Ngarenairobi na Kata ya Gararagua ambayo ni mojawapo kati ya Kata tatu zinazofanya Uchaguzi kwa ajili ya kumchagua Mbunge na Diwani. 

Kwa ujumla maandalizi kwa ajili ya upigaji Kura yamekwenda vizuri licha ya changamoto ya kuchelewa kufunguliwa kwa baadhi ya vituo kulikochangiwa na umbali wa vituo huku wengi wa Mawakala wakieleza kuridhishwa na Mchakato mzima wa kuanza kwa Upigaji Kura.

Aidha katika baadhi ya vituo ambavyo NEC TV imetembelea Wasimamizi Wasaidizi wameonekana kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu pamoja na maelekezo mengine ya Tume yakiwemo ya kuwaruhusu Wazee, Wagonjwa na Wakina mama wenye watoto wadogo kutosimama kwenye mistari na badala yake kwenda moja kwa moja kupiga kura.

Jimbo la Uchaguzi la Siha ni miongoni mwa Majimbo 2 yanayofanya Uchaguzi wa Mbunge pamoja na Madiwani katika Kata 3 kufuatia Uchaguzi Mdogo uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanyika Februari 17, mwaka huu. Jimbo linguine linalofanya Uchaguzi wa Mbunge ni Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment