TANGAZO


Thursday, February 1, 2018

Iron Biby: Alichekwa kwa kuwa mnene utotoni lakini sasa ni bingwa wa kunyanyua uzani

Cheick Ahmed al-Hassan Sanou

Haki miliki ya pichaCHEICK SANOU
Image captionWakati alipotimiza umri wa miaka tisa, Cheick alikuwa amezoea kukejeliwa na kutaniwa
Cheick Ahmed al-Hassan Sanou alikuwa na uzito wa kupindukia kila wakati, lakini hakujua ni kwa kiasi gani ana nguvu mpaka siku ile alipomtupa mmoja watu waliokuwa wakimkejeli hadi upande mwingine wa chumba.
Hii ni habari ya namna kijana aliyezomewa aligeuka na kuwa mshiriki wa mashindano ya mtu mwenye nguvu zaidi duniani.
Ikiwa una miaka 16, na kilo za mwili 122 na kifua upana wa inchi 48 kuna uwezekano mkubwa wa kuonekana mnene zaidi ya wengine na hivyo ndivyo ilikuwa kwa Cheick Ahmed al-Hassan Sanou.
Sanou ambaye alizaliwa Burkina Faso 1992, Biby kama anavyopendwa kuitwa, alitambua kuwa alikuwa tofauti na ndugu zake alipokuwa na umri wa miaka mitano na hilo lilikuwa ni jambo ambalo kidogo lilimtatiza.
"Mama yangu alisema nilikuwa mnene tangu nilipozaliwa- nikiwa na kilo 5 na nilikuwa nikivuta pumzi kwa nguvu -sio kama mtoto mchanga wa kawaida," alitabasamu alipokuwa akielezea maisha yake ya utotoni.
"Nilitaka kuwa mkimbiaji wa mbio fupi maana nilikuwa na kasi ya kukimbia hata kama nilikuwa mzito," aliiambia BBC.
"Lakini kila mara nilipokuwa nikikimbia, mwili wangu ulikuwa unatikisika, na watoto wenzangu shuleni walikuwa wakicheka sana na kuniita 'Fat Boy'. Ilikuwa ni kama burudani kwao, kwa hiyo nikakata tamaa, lakini sikuwahi kuacha nia yangu ya kuwa mwanariadha''.
Kila mara uigizaji na sarakasi pia zilimvutia, lakini kila alipofanya sarakasi yoyote sauti ya mwili wake ukigonga zulia na ilipokelewa na watu kwa kejeli kuashiria kuwa alikuwa hawezi.
Cheick Ahmed al-Hassan SanouHaki miliki ya pichaCHEICK SANOU
Image caption"Watu hawakuwa wanene sana nchini Burkina Faso, na wasichana waliokuwa na umri sawa na wangu walipenda vijana wembamba'' alisema
Wakati alipotimiza umri wa miaka tisa, Cheick alikuwa amezoea kukejeliwa na kutaniwa.
Nilijichukia kwa kuwa hivyo - nilikuwa mdogo zaidi katika darasa langu, lakini nilionekana mkubwa kwa miaka minne zaidi ya wenzangu wakiwemo kaka zangu.
"Watu hawakuwa wanene sana nchini Burkina Faso, na wasichana waliokuwa na umri sawa na wangu walipenda vijana wembamba.
Wasichana wakubwa walikuwa wanazungumza nami na kuwa wakarimu, lakini nilipoonyesha aina yoyote ya kutaka urafiki nao walikua wanakataa''
Alivumilia matusi na udhalilishaji bila kukabiliana na yeyote hadi alipofika umri wa kubalehe wakati ambapo aligundua ana nguvu kwa kiwango gani - la kushangaza ilikuwa ni kwa kijana mkubwa ambaye alikuwa akimchokoza.
CHEICK SANOU
CHEICK SANOUHaki miliki ya pichaCHEICK SANOU
Image captionMwaka 2009, Cheik mwenye umri wa miaka 17 alitumwa nchini Canada kukamilisha masomo yake ya sekondari huko alikuwa maarufu kwa kunyanyua uzani wa juu
"Nilikasirika nikasema: 'niache , nikamsukuma mbali, lakini alipaa hadi upande miwingine wa chumba na akashtuka.
Nilishtuka pia, lakini nikajua siku ile kuwa nina nguvu - hakunisumbua tena ."
Wakati mmoja kaka yake alisafiri kwenda Canada mwaka 2007, alimuomba amtumie kifaa cha kukondesha mwili alichokiona kwenye tangazo la kibiashara kwenye jarida lililoahidi wateja kuwa miili yao itakonda.
Lakini kwa kuwa kaka yake hakuweza kupata kifaa hicho alibakia kuwa mnene na mwenye shauku ya kupoteza kilo za mwili.
Kila mbinu aliyoitumia kupunguza uzito wa mwili hakufanikiwa.
Halafu mwaka 2009, Cheik mwenye umri wa miaka 17 alitumwa nchini Canada kukamilisha masomo yake ya sekondari.
Kwenda kwake kulimfanya awe na malengo mapya ya kupoteza uzito . Alijiunga na mazoezi ya mwili (gym) katika siku yake ya kwanza, lakini kitu fulani kilikuwa karibu kutokea ambacho kingemuathiri katika maisha yake yaliyosalia.
Alichaguliwa kama mmoja wa wachezaji wa timu ya kikapu - na kwa mara ya kwanza maishani mwake, alifanya kitu ambacho alikijali sana.
CHEICK SANOUHaki miliki ya pichaCHEICK SANOU
Image captionMwaka 2013, aliingia shindano la kwanza la wanyanyuaji wa uzito mkubwa na akashinda, ukafuatia ushindi katika mashindano ya kitaifa baadaye katika mwaka huo
Kwa kipindi kifupi Cheick alikuwa maarufu katika eneo la kufanyia mazoezi, akinyenyua uzito sawa na wanyanyuaji vyuma wenye taaluma hiyo.
Mnamo mwaka 2013, aliingia shindano la kwanza la wanyanyuaji wa uzito mkubwa na akashinda, ukafuatia ushindi katika mashindano ya kitaifa baadaye katika mwaka huo.
"Kaka yanyu alikua akiniita Iron Biby (Chuma Biby) na jina hili limenifuata kote ninakoenda, lakini nilipoanza kufahamika kwa kunyanyua uzani wa juu nikawa Iron Biby," alikumbuka.
Mashindano ya kimataifa yakafuata kwa hiyo akawa Chuma Biby kweli.
Kwa mtu mgeni, Iron Biby ni mshindani kwani tayari amekwishawapiku watu maarufu kwenye matukio wayapendayo, na hajalenga kukomea hapa.
"Mpango wangu ni kuwa binadamu imara zaidi duniani na kuchukua taji la Burkina Faso," alisema.
Kuonekana kwa udhabiti wake kumewafanya vijana wa Burkina Faso kutamani kuwa kama yeye.
Wengi miongoni mwao ambao walikuwa wakiwatamani kuwa wachezaji soka sasa wanataka kuwa wanaume wenye nguvu(ama wanawake thabiti).

18 comments:

  1. eset-nod32-antivirus-license-key-full the list of features of Bitcoin Monitoring, Banking Protection, and Control. ESET's user interface is better and newer this season. We think last year's version is more. NOD32 Antivirus,
    new crack

    ReplyDelete
  2. Amazing blog! I really like the way you explained such information about this post with us. And blog is really helpful for us. virtual-dj-crack

    ReplyDelete
  3. Microsoft Office 2019 Crack is a program that assists individuals with further developing their composing abilities. It has been generally welcomed by PC clients who have viewed it as a compelling instrument in further developing exactness and speed.

    ReplyDelete
  4. Hello Everyone this page has usefull information,as i found the content in post this also have the relative ideas, Thanks...!!
    tunefab spotify music converter crack
    pc reviver crack

    ReplyDelete
  5. Hello Everyone this page has usefull information,as i found the content in post this also have the relative ideas, Thanks...!!
    Blue Iris Crack
    IZotope RX 8 Audio Editor Advanced Crack
    Airmail crack
    Tvpaint Animation crack
    IDM Crack

    ReplyDelete
  6. UPSC Exam or IAS Exam is known as the UPSC Civil Services Examination (CSE). It is conducted by the Union Public Service Commission to recruit students into various civil service in India.












    ReplyDelete
  7. I'd love to be a member of a group where I can obtain advice from folks who have gone through similar experiences as me. Please do not hesitate to contact me if you have any suggestions or thoughts. Your assistance has been much appreciated.
    Winthruster Crack
    ManyCam Crack
    TeamViewer Crack
    WinRAR Crack

    ReplyDelete
  8. I am very thankful for the effort put on by you, to help us, Thank you so much for the post it is very helpful, keep posting such type of Article.
    Adobe Photoshop CS5 Extnded Crack
    AutoCad 2018 Crack
    Zoom Pro Crack
    DriverFix Pro Crack

    ReplyDelete