Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita.
|
Wananchi wa Kata ya Nkome wakiwa kwenye mkutano ambao ulikuwa na lengo la kuelezea hali ya uvuvi haramu ilivyo kwenye kata ya Nkome na namna ambavyo oparesheni imeweza kufanyika kwenye maeneo hayo.
|
Kiongozi wa kikosi
maalumu kinachoendesha oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu ziwa victoria
Gabriel Mageni akielezea namna ambavyo wameweza kuendesha zoezi hilo ndani ya siku kumi na mbili.
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi akisisita kwa wale ambao ni watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu.
Na Joel Maduka, Geita.
|
SERIKALI Mkoani Geita Imeteketeza zana haramu
zenye thamani ya shilingi milioni therathini na tatu zikiwemo Nyavu za makila zilizounganishwa 2,393,makokolo ya sangara
32,timba 142 makokoro ya dagaa 7 na dududu 11.
Hatua hiyo
imetokana na oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo
inaendelea kwenye maeneo ya ziwa viktoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi huo ndani ya ziwa hilo pamoja na kuondoa
mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki
wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume
cha sheria.
Zoezi hili
la uteketezaji zana hizo limefanyika kwenye Kata ya Nkome ,ambapo kiongozi wa
oparesheni hiyo Gabriel Mageni
,amemweleza mkuu wa mkoa huo kwamba kuna baadhi ya wafanyakazi wa hifadhi ya Rubondo wamekuwa wakihusika na uvuvi haramu kwa
kuwaruhusu wavuvi kuingia kwenye hifadhi
na wengine kuficha zana zao ndani ya hifadhi na kwamba wamekuwa
wakilipwa fedha wafanyakazi hao maarufu kwa jina la "KIFUNDA"
Kufuatia
malalamiko hayo mtandao huu umetafuta kwa njia ya simu afisa mahusiano wa
TANAPA Pascal Shelutete alisema kuwa wao kama watu ambao wanamamlaka ya hifadhi
za taifa na kwamba kwa mujibu wa kanuni na taratibu za sheria askari wao hawapaswi kushiriki kwenye vitendo
vya ujangili na kwamba taratibu za kiuchunguzi zikifanyika na wakabaini kuna
watumishi wanajihusisha na vitendo hivyo hatua za kisheria na za kinidhamu
zitachukuliwa na hawawezi kuwakingia kifua.
Aidha Mageni
aliongeza kuwa katika operesheni hiyo
ambayo ina siku kumi na mbili baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa
wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni wanaojishughulisha
na shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha serikali kukosa
mapato.
Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Robert
Luhumbi, amewataadhalisha watendaji ambao
wanashirikiana na wavuvi haramu na kwamba endapo kuna mtu hakibainika na
kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua na kwamba kupitia
oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo.
Nyawalwa
Wange ni moja kati ya watu ambao
wanajishughulisha na kazi ya uvuvi alisema agizo la Mkuu wa Mkoa ni la kuungwa mkono
kutokana na kwamba uvuvi haramu umeendelea kuharibu kwa kiasi kikubwa samaki
ambao wapo ndani ya ziwa viktoria na kwamba serikali iendelee kuwabaini wale
wote ambao wanaendelea kufanya shughuli za uvuvi kinyume na sheria.
Katika
oparesheni hiyo jumla ya fedha ambazo zimekusanywa ni zaidi ya milion, 111 fedha
zinazotokana na faini ,malipo ya mrahaba pamoja na mauzo ya samaki.
No comments:
Post a Comment