TANGAZO


Monday, January 22, 2018

MIFUKO 3000 SARAJI YACHANGWA KUKAMILISHA USHINDI SEMINARI

Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzanaia Askofu Dkt. Barnabas Mtokambali

Na Tiganya Vincent
RS-Tabora 
22 Januari 2018
VIONGOZI mbalimbali wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) na Seriakali Mkoani Tabora wameahidi kutoa mifuko 3000 ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Shule ya Seminari ya Ushindi inayojengwa katika eneo la Kipalapala kwenye Manispaa ya Tabora.

Akizungumza jana mjini Tabora kabla ya zoezi hilo la harambee kuanza Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzanaia Askofu Dkt. Barnabas Mtokambali alisema kuwa Kanisa limeamua kujenga Shule mbalimbali ili kutoa mchango katika kupiga vita umaskini , maradhi na ujinga.

Alisema kuwa Kanisa linachukua hatua hiyo kwa kutambua kuwa silaha kubwa ya kupambana na maadui hao watatu ni elimu ndio maana pamoja na kutoa huduma nyingine katika jamii kama vile afya na maji pia wawekeza katika kujenga kujenga ili kuelimisha jamii.

Askofu Mkuu wa TAG Askofu Dkt.Mtokambali alisema kuwa Viongozi wa Kanisa na watu wengine kama wazazi wanalojukumu la kuwasaidia watoto kuwapata elimu bora na yenye maadili itakayowasaidia kupiga vita umaskini, ujunga na maradhi.

Alisema kuwa elimu bora na yenye maadili itamwezesha mtoto kuweza kutawala mazingira yake ambayo yatamasaidia kuondoa maadui hao watatu.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za Mkoa wakati wa zoezi hilo , alisema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa madhehebu yote na wadau mbalimbali wanaungana na Serikali katika kutoa huduma mbalimbali ikiwemo elimu na afya.

Alisema kuwa atahakikisha kuwa vikwazo vyote ambavyo vichelewesha upatikanaji wa huduma hizo kwa jamii vinaondolewa haraka ili wananchi waweze kunufaika haraka na huduma zilizopangwa kutolewa.

Awali Mkurugenzi wa akielezea maendeleo ya ujenzi wa Seminari ya Ushindi alimuomba Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha anawasaidia kuwatambulisha kwa uongozi wa elimu mkoani humo ili waweze kufanyakazi kwa karibu zaidi.

Alisema kuwa  Idara ya Elimu ya TAG mkoani Tabora imekuwa haifanyi vizuri katika baadhi ya shule kwa sababu ya kukosa ushirikiano kwa watendaji wa sekta ya elimu.

No comments:

Post a Comment