Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) (hawapo pichani) unaotarajia kufanyika nchini mwezi Februari 2018 kuhakikisha maandalizi yanakuwa mazuri ili ujio huo uwezekuletea manufaa kwa taifa katika kikao kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.(Picha zte na Anitha Jonas – WHUSM)
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) wakisililiza maagizo ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliyokuwa akitoa katika kikao hicho kwa lengo la kufanikisha ujio huo wa Kimataifa kuwa unaleta manufaa kwa taifa jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe katika kikao cha maandalizi ya ujio huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Yusuph Singo.
No comments:
Post a Comment