Mkufunzi wa Borussia Dortmund Peter Stoger anasema kuwa hakuna ombi la kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang lililowasilishwa na Arsenal.
Mshambuliaji huyo wa Gabon ambaye ananyatiwa na the Gunners, hakusafiri na wachezaji wenzake kwa mechi ya Ijumaa dhidi ya Hertha berlin ambayo ilikamilika 1-1.
"hakuna mazungumzo yoyote katika meza kuhusu uhamisho wa Aubameyang, yanayoendelea ni uvumi. alisema Stoger.
"Tunapanga na Pierre-Emerick Aubameyang na kuna vile atakavyorudi katia kikosi cha kwanza cha timu ."
Aubameyang pia alikosa mechi ya Jumapili iliotoka sare ya 0-0 dhidi ya Wolfsburg baada ya kukosa kuhudhuria mkutano wa timu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ni mshambuliai wa Dortmund mwenye magoli mengi msimu huu akiwa na mabao13 katika mechi 15 .
No comments:
Post a Comment