TANGAZO


Friday, December 8, 2017

Papa Francis anataka maombi ya Baba Yetu yarekebishwe

Pope greets crowds at audience on 8 November

Haki miliki ya pichaREUTERS
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba maombi maarufu ya Kikristo ya Baba Yetu yafanyiwe marekebisho.
Anataka sehemu ambayo huzungumzia vishawishi ilitafsiriwa vibaya.
Asema tafsiri kwamba "Usitutie katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" iangaziwe upya akisema tafsiri iliyofanywa si sahihi kwa sababu Mungu huwa hawaongozi binadamu kutenda dhambi.
Papa amependekeza watu watumie "usituache tukaingia katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" badala yake.
Alitoa pendekezo hilo akizungumza katika runinga ya Italia Jumatano usiku.
Ombi la Baba Yetu ndilo linalofahamika vyema zaidi miongoni mwa maombi ya Kikristo.
Papa Francis amesema Kanisa Katoliki nchini Ufaransa sasa linatumia tafsiri hiyo ya "usituache tukaingia katika vishawishi" kama mbadala, na kwamba jambo kama hilo linafaa kufanywa kote duniani.
"Usiniache nikaingia kwenye vishawishi kwa sababu ni mimi nitakayeanguka, si Mungu anayetutia katika vishawishi na kisha kutazama nilivyoanguka," aliambia runinga ya TV2000, runinga ya kanisa Katoliki Italia.
"Baba hawezi kufanya hivyo, baba hukusaidia huinuke upesi."
Pope Francis meets a group of Rohingya refugees in Dhaka, Bangladesh December 1, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPapa Francis alipokutana na wakimbizi wa Rohingya mjini Dhaka, Bangladesh Desemba 1, 2017
Ni tafsiri kutoka kwa tafsiri ya biblia ya Kilatini ya karne ya nne ambayo iliidhinishwa rasmi na kanisa Katoliki karne ya 16, ambayo ilitafsiriwa kutoka kwa maandiko ya kale ya Kigiriki, Kiebrania na Kiaramaic.
Tangu kuanza kuhudumu kama Papa, Papa Francis hajasita kugusia masuala tata na amekabiliana na baadhi ya mambo moja kwa moja, wachanganuzi wa mambo ya Vatican wanasema.
Alikuwa awali amesema kwamba Kanisa Katoliki linafaa kuwaomba radhi wapenzi wa jinsia moja kutoka na vile ambavyo limewatazama na yale limewatendea kwa miaka mingi.
Aidha, alilinganisha vituo vya kuwazuilia wahamiaji Ulaya na vituo vilivyotumiwa na Wanazi kuwazuilia na kuwaua Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

No comments:

Post a Comment