TANGAZO


Friday, September 1, 2017

Sababu ya Alexis Sanchez kukosa kuondoka Arsenal

Sanchez

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Juhudi za klabu ya Manchester City kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez ziligonga mwamba siku ya mwisho ya kuhama kwa wachezaji baada ya Gunners kukosa mchezaji wa kujaza nafasi yake.
Inaarifiwa kwamba City na Arsenal walikuwa wamefikia makubaliano, kwa masharti hata hivyo, kuhusu kuhama kwa Sanchez, 28, hadi Etihad.
Ada ya uhamisho wake ilikuwa £55m, na vikolezo vya £5m, lakini ilitegemea kufanikiwa kwa Arsenal kumpata mchezaji wa kujaza nafasi yake.
Mchezaji waliyemtaka zaidi alikuwa winga wa Monaco Thomas Lemar ambayo inadaiwa alikataa kuhamia Arsenal.
Monaco walikuwa wamekubaliana na Arsenal kuhusu uhamisho wa Lemar, 21, ambaye huchezea timu ya taifa ya Ufaransa kwa £90m.
Sanchez alitaka kujiunga na City ambapo angeunganishwa tena na meneja wake wa zamani alipokuwa Barcelona Pep Guardiola.
Mchezaji huyo wa Chile anatumikia mkataba wake wa mwisho Emirates na kuna uwezekano mkubwa kwamba ataondoka majira yajayo ya joto bila kulipwa ada yoyote.
Mchezaji aliyendoka Emirates siku ya mwisho ni mshambuliaji Lucas Perez, ambaye alijiunga nao msimu uliopita kwa £17.1m.
Perez alirejea klabu yake ya awali Deportivo La Coruna kwa mkopo baada ya kufunga mabao saba katika mechi 21 alizowachezea Gunners.

Uchanganuzi

Kiungo wa kati wa Stoke Charlie Adam akizungumza na BBC Radio 5:
Arsenal wanamhitaji Alexis Sanchez zaidi ya wanavyohitaji £60m.
Bila yeye, hawana nafasi ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Baada ya kumalizika kwa kipindi cha kuhama wachezaji, atatulia na kujitolea tena kwa msimu mwingine.
Kiungo wa kati wa zamani wa Aston Villa, Chelsea naJamhuri ya Ireland Andy Townsend:
Arsenal wamo taabani. Ningemwacha Sanchez aende.
Ishara alizoonyesha baada ya Arsenal kushindwa 4-0 na Liverpool hazikuwa nzuri.
Amechoka na fikira zake ziko kwingine. Sidhani atayasahau yote na kurejea haraka kuwachezea kama kawaida.
Mwanachama wa bodi ya mashabiki, Arsenal Supporters' Trust Akhil Vyas:
Naomba arudi kuangazia tena timu na kujitolea kabisa, jambo ambalo hufanya akiwa uwanjani, kwa msimu huu angalau.
Dirisha la kuhama wachezaji limefungwa kwa masikitiko, iwapo hatumnunui mchezaji mwingine, basi ilikuwa lazima tusalie na Alexis.
SanchezHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSanchez aliwachezea Arsenal mechi waliyolazwa 4-0 na Liverpool Jumapili

Kuhama kutoka Barca

Sanchez alichezea Arsenal mara ya kwanza msimu huu mechi waliyolazwa 4-0 na Liverpool Jumapili.
Sanchez alijiunga na Arsena kutoka Barcelona mwaka 2014 kwa ada ya takriban £35m na alishinda kombe lake la pili ya FA akiwa na Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita.
Mapema mwezi huu meneja wa Arsenal Arsene Wenger alisema Sanchez anataheshimu uamuzi wake wa kutaka kusalia naye mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake.
Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool na England Danny Murphy amesema Arsenal hawawezi kuthubutu kumwachilia.
"Wakimwacha aende watakuwa katika matatizo chungu nzima. Bado wako kwenye matatizo makubwa kwa kiasi fulani tayari.
"Alifanya kazi kwa bidii sana (mechi dhdii ya Liverpool) lakini mechi ilipoanza kuwalemea Arsenal, ungemuona alionekana kukata tamaa.
Awali, Arsenal walikuwa wamekataa majaribio yoyote ya kutaka kumchukua Sanchez kufikia na iliaminika kwamba wangefurahia sana iwapo Raheem Sterling angekuwa kwenye sehemu ya mkataba wake wa kuhamia City.
Meneja wa City Pep Guardiola hata hivyo alitaka kumnunua Sanchez, 28, moja kwa moja.
Hata hivyo, hatua ya kumnunua ingewezaweza kutilia shaka mustakabali wa Raheem Sterling katika City.
Sterling, 22, anayechezea timu ya taifa ya England amechezea City mechi zao zote tatu za kwanza ligini msimu huu.
Lakini hangehakikishiwa nafasi ya kuanza mechi Etihad hasa baada ya kuwasili kwa Bernardo Silva kutoka Monaco.
BBC ilikuwa imefahamu kwamba Sterling anaweza kufurahia kwenda Arsenal na kurejea jijini London iwapo angekuwa kwenye sehemu ya mkataba wa kumchukua Sanchez.

No comments:

Post a Comment