TANGAZO


Friday, September 1, 2017

LIGI SOKA YA "DEFAO CUP 2017" YAZINDULIWA IKUNGI MKOANI SINGIDA

BMG Habari, Pamoja Daima! 
UZINDUZI wa ligi soka ya Defao CUP 2017 umefanyika katika Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida kwa kushirikisha jumla ya timu nane ambazo ni Minyinga, Makiungu, Mungaa, Unyaghumpi, Siye, Kinku, Wibia pamoja na Unyang'ongo. 

Katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo, timu ya Unyaghumpi ilikubali kipigo cha bao 2-0 kutoka timu ya Wibia. Mwandaaji wa ligi hiyo, Salumu Mtaturu maarufu kwa jina la Defao, alisema lengo lake ni kuhamasisha vijana wilayani Ikungi hususani Kata shiriki za Makiungi, Mungaa na Puma ili kutazama fursa zilizopo kwenye Kata zao na kuzitumia ipasavyo kwa ajili ya matokeo chanya ya kimaendeleo.

"Lakini pia tumelenga kutafuta kikosi kitakachojumuisha vijana kutoka Kata zinazoshiriki ligi hii ili tuweze kuunda timu ya vijana itakayoweza kushiriki ligi mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya ambapo tayari tumeanza taratibu za usajili wa timu hiyo". Alisema Defao. 

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo uliofanyika Oktoba 25,2017 alikuwa diwani wa Viti Maluumu Zainabu Khamis aliyeongozana na viongozi mbalimbali akiwemo diwani wa Kata ya Puma na Wenyeviti wa Vijiji vya Makiungi, Wibia pamoja na Unyang'ongo. 

"Niwaase vijana kutumia mashindano haya kama chachu ya kujitoa kwenye makundi yasiyo na tija katika jamii yakiwemo ya uvutaji bangi". Alisema mgeni rasmi huku akimpongeza kijana Defao (20) ambaye ni mhitimu wa chuo kwa kuanzisha ligi hiyo. 

Wadau mbalimbali wa michezo wanahimizwa kujitokeza kuongeza nguvu kwenye michuano hiyo hususani kwenye suala la zawadi ambapo hadi sasa zawadi zilizopangwa ni mbuzi pamoja na mpira mmoja kwa ajili ya mshindi wa kwanza, mshindi wa pili mpira mmoja pamoja na Tsh.20,000 huku mshindi wa tatu akijishindia mpira mmoja. 
Kijana Defao akizungumza kwenye uzinduzi wa ligi ya Defao Cup 2017. Viongozi mbalimbali wakikagua timu. Bonyeza BMG Habari, Pamoja Daima kutazama uzinduzi wa ligi ya IKUNGI ELIMU CUP 2017.

No comments:

Post a Comment