Rais wa Somalia Mohamed Farmajo ameamrisha uchaguzi kufanyika kufuatia kisa ambapo vikosi vya usalama nchini humo vilifyatuliana risasi siku ya Jumatano na kusababisha vifo vya wanajeshi wanne.
Maafisa wa kijeshi katika kizuizi kimoja cha ukaguzi waliwafyatulia risasi maafisa wa ujasusi ambao hawakuwa wamevaa sare rasmi.
Kisa hicho kiliashiria matatizo yaliyopo kwenye ushirikiano katika ya vikosi vya usalama kwenye mji mkuu Mogadishu.
- Trump aongeza mashambulizi zaidi dhidi ya Al Shabab
- Somalia yailalamikia Marekani kuhusu mashambulio
- Jeshi la Marekani lasaidia jeshi la Ufilipino kupigana na wanamgambo
Taarifa zinasema kuwa mapigano yalizuka wakati wanajeshi walizuia msafara ulikuwa ukimsafirisha afisa wa zamani wa ujasusi.
Maafisa wote waliohusika wamekamatwa na polisi wanachunguza video za CCTV.
Katika tukio jingine mwezi Mei waziri wa serikali aliuawa baada ya wanajeshi kuuufyatulia risasi magari yake karibu na ikulu ya Rais.


No comments:
Post a Comment