TANGAZO


Wednesday, July 19, 2017

Wafanyakazi wanaolipwa mishahara ya juu zaidi katika BBC wafichuliwa

Chris Evans and Claudia Winkleman

Haki miliki ya pichaPA/GETTY IMAGES
Image captionEvans na Winkleman ndio wanalipwa zaidi upande wa wanaume na wananawake
Chris Evans amekuwa wa kwanza katika orodha ya wafanyakazi nyota wa BBC wanaolipwa mishahara ya juu zaidi.
Alilipwa kati ya pauni milioni 2.2 na milioni 2.25 mwaka 2016/2017, huku Claudia Winkleman akiwa mwanamke mfanyakazi nyota wa BBC anayelipwa mshahara wa juu zaidi, akiwa anapiliwa kati ya pauni 450,000 na 500,000.
Karibu thuluthi mbili ya nyota wanaolipwa zaidi ya pauni 150,000 ni wanaume ikilinganishwa na thuluthi moja ya wanawake.
BBC pay graphic
Image captionMalipo ya baadhi ya wafanyakazi wa BBC
Mkurugenzi mkuu wa BBC Tony Hall alisema kuwa kuna mengi yanahitaji kufanywa kwa suala ya jinsia.
Viwango ambavyo vimetolewa katika ripoti ya kila mwaka ya BBC, vinafichukua mwanya wa malipo ulio kati ya wanawake na wanaume.
Kwa ujumla wanaume25 wanaofaya kazi inayohitaji vipawa, hulipwa zaidi ya pauni 250,000 ikilinganishwa na wanawake tisa tu.
The judges on Strictly Come Dancing
Image captionWawili kati ya majaji wa kipindi cha Strictly wanalipwa zaidi kuliko wengine
Hii ndiyo mara ya kwanza mishahara ya wafanyakazi nyota wa BBC wanaolipwa zaidi ya pauni 150,000 imetangazwa kwa umma.
Ripoti hiyo ya kila mwaka hata hivyo haijatoa kiwango kamili cha mishahara na pia haijajumuisha wafanyakazi nyota ambao hupokea mishahara kutoka BBC Worldwide.
Pia orodha hiyo haikutofautisha mishahara ya watu wanaofanya kazi zaidi ya moja ndani ya BBC na wale walio na kazi moja.
BBC pay graphic
Image captionWanaolipwa zaidi

No comments:

Post a Comment