Roboti ya chini ya maji imenasa picha zinazoaminika kuwa za kwanza kabisa ya mafuta ya nuklia yaliyoyeyuka ndani ya kinu cha Japan kilichoharibiwa cha Fukushima.
Viwango vikubwa vya vitu vinayoonekana kama mawe vimeonekana katika kinu chake cha tatu.
Ikiwa itathibitishwa itakuwa mafanikio makubwa katika oparesheni ya kusafisha kinu hicho.
AFP
Kinu hicho kulikumbwa na tsunamni mwaka 2011 na kusababisha ajali mbaya zaidi ya kinu cha nuklia tangu ile ya Chernobyl.
Zaidi ya watu 200,000 walilazimika kuhama makwao kutokana na uchafuzi uliotokana na kinu hicho.
Baadhi ya maeneo yaliyoharibiwa bado yana uchafu mbaya wa nuklia na roboti hutumiwa kuyasafisha.
AFP
Ugunduzi huo ulifuatia uchunguzi wa siku tatu wa kutumia roboti ndogo ya chini ya maji inayoitwa Little Sunfish.
Zaidi ya watu 18,500 waliuawa au kutoweka wakati tetemeko la ardhi lilisababisha tsunami kubwa ambayo ilisababisha ajali katika kinu cha Fukushinm.
(C) BRITISH BROADCASTING CORPORATION


No comments:
Post a Comment