TANGAZO


Saturday, July 29, 2017

Kim Jong-un: Tunaweza kushambulia eneo lolote Marekani

Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanyia jaribio kombora lake la masafa marefu ICBM, wakitaja kuwa onyo kali kwa Marekani

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKorea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanyia jaribio kombora lake la masafa marefu ICBM, wakitaja kuwa onyo kali kwa Marekani
Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanyia jaribio kombora lake la masafa marefu ICBM, wakitaja kuwa onyo kali kwa Marekani.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisema kuwa jaribio hilo lilibaini kwamba marekani yote ipo katik radara ya Korea Kakazini na sasa inaweza kushambuliwa, vyombo vya habari vimeripoti.
Jaribio la kombora hilo linajiri wiki tatu baada ya jaribio la kombora la kwanza la masafa marefu la Korea Kaskazini.
Rais wa Marekani Donald Trump amelitaja jaribio hilo kuwa la kijinga na kitendo cha hatari kilichotekelezwa na utawala wa Korea Kaskazini.
China pia imeshutumu jaribio hilo huku ikitaka pande husika zilizo na wasiwasi kujizuia ili kutoendeleza wasiwasi zaidi.
Ikithibtisha kurushwa kwa kombora hilo, Korea Kaskazini ilisema kuwa kombora hilo la masafa marefu liliruika kwa dakika 47 na kufika urefu wa kilomita 3,724

No comments:

Post a Comment