TANGAZO


Friday, July 21, 2017

Kasuku atamka maneno ya mwisho ya mwanamme aliyeuwawa na mkewe

Glenna and Martin Duram pictured

Haki miliki ya pichaABC
Image captionGlenna Duram amepatikana na hatia ya kumuua mumewe Martin
Mwanamke amepatikana na hatia ya kumuua kwa kuimpiga risasi mumewe mara tano katika jimbo la Michigan kwenye kisa ambacho kilishuhudiwa na kasuku.
Glenna Duram alimpiga risasi mumewe mbele ya kasuku huyo mwaka 2015 na kisha akajaribu kujiua kwa kujipiga risasi.
Kasuku huyo anayejulikana kama Bud, baadaye alirejelea maneno "usipige risasi" kwa sauti ya muathiriwa, kwa mujibu wa mke wa zamani wa Duram.
Hata hivyo kasuku huyo hakutumiwa wakati wa kesi mahakamani.
A stock photo of an African Grey parrot
Image captionKasuku sawa na huyu ana uwezo mkubwa wa kuiga sauti
Jaji alimpata Bi Duram 49, na makosa ya mauaji na atahukumiwa mwezi ujao.
Alipata majeraha ya kichwa wakati wa kisa hicho kilichotokea nyumbani kwao mwezi Mei mwaka 2015.
Mke wa zamani wa Duram Christina Keller, ambaye sasa anamiliki Kasuku Bud, mapema alisema anaamini chiriku huyo alikuwa akirejelea mazungumzo ya kutoka usiku wa mauaji ambayo anasema yaliishia kwa kusema "usipige risasi"

No comments:

Post a Comment