Wakati udukuzi wa mitandao wanapoendesha udukuzi zaidi, China inatarajiwa kuzindua mtandao usiodukuliwa ikimaanisha kuwa itakuwa rahisi kugundua kabla ya wadukuzi kuingia.
Mradi huo wa kichina katika mji wa Jinan na unautumia teknolji inayofahamika kama Quantum, unajawa kuwa hatua kubwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo.
Mradi huo pia ni ishara tosha kuwa China inachukua wajibu mkuwa katika masuala ya teknolojia ambayo kwa miaka mingi yametawaliwa na nchi za magharibi.
- Ukrain: Urusi ilihusika na udukuzi wa mitandao
- Urusi yawakamata wataalamu wa mitandao kwa kusaliti nchi
- Twitter na mitandao mingine yavamiwa
Kupitia mtandao huo wa Jinan, watumiaji 200 kutoka jeshi, serikali, sekta ya fedha na kawi wataweza kutuma ujumbe kwa njia salama.
Hatua hii inamaana kuwa China inachukua hatua kubwa kuhakikisha kuwa mitandao imekuwa salama. Sasa huenda nchi zingine zikanunua teknolojia hii kutoka China.
SPL


No comments:
Post a Comment