TANGAZO


Tuesday, July 25, 2017

BALOZI SEIF IDDI AMFARIJI MWAKILISHI WA JIMBO LA UZINI MOHAMED RAZA ALIYEKUWA NCHINI INDIA KWA MATIBABU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kulia) akimfariji Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Mohamed Raza Hassanali hapo Hotelini Kwake Golden Tulip Kibweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Mh. Raza anaendelea na mapumziko mafupi baada ya kufanyiwa matibabu Nchini India hivi karibuni. Aliyepo nyuma yao ni mdogo wake, ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kimbesamaki Mh. Ibrahim Raza.(Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ) 
Mh. Mohamed Raza kati kati akieleza namna alivyopata huduma za Afya wakati akiwa Hospitalini Nchini India. Wa kwanza kulia ni Balozi Seif na kulia ya Mheshimiwa Raza ni Daktari Azan anayefuatilia afya yake katika kipindi hichi cha mapumziko.  
Dr. Azan akimueleza Balozi Seif baadhi ya njia anazopaswa Mtu kuzichukuwa  katika kujilinda dhidi ya maradhi ya Kisukari makubwa zaidi ni kufuata miko ya vyakula na kufanya mazoezi kila siku.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kulia) akizungumza na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Mohamed Raza Hassanali hapo hotelini kwake Golden Tulip, alipokwenda kumfariji, Kibweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 
Dr. Azan akimueleza Balozi Seif baadhi ya njia anazopaswa Mtu kuzichukuwa  katika kujilinda dhidi ya maradhi ya Kisukari makubwa zaidi ni kufuata miko ya vyakula na kufanya mazoezi kila siku.

No comments:

Post a Comment