Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akisalimiana na Kiongozi wa Timu ya Madaktari kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha El – Shady Alexandria Nchini Misri Profesa Saber Waheeb waliopo Zanzibar kutoa huduma za Upasuaji. (Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)
Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Timu ya Madaktari kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha El – Shady Alexandria Nchini Misri unaoongozwa na Profesa Saber Waheeb. Kiongozi wa Timu ya Madaktari kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha El – Shady Alexandria Nchini Misri akimpatia zawadi Balozi Seif baada ya kumaliza mazungumzo yao. Katikati yao ni mratibu wa TImu hiyo ambaye pia ni muwekezaji wa miradi tofauti ya kiuchumi nchini Misri, Bwana Karam Kordy.
Picha no:- 953 ni:- Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Madaktari wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha El – Shady Alexandria Nchini Misri baada ya kumaliza mazungumzo yao. Kushoto kwa Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Afya Mh. Harous Said Suleiman, Balozi wa Tanzania Nchini Misri Balozi Mohamed Haji Hamza na Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Ali Salum Ali. Kulia kwa Balozi Seif ni Kiongozi wa Madaktari kutoka Nchini Misri Profesa Saber Waheeb, Mratibu wa Timu Hiyo Bwana Karam Kordy na Mke wa Profesa Saber Waheeb.
Juu na Chini ni baadhi ya Madaktari hao wakiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi.
Juu na Chini ni baadhi ya Madaktari hao wakiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi.
Juu na Chini ni baadhi ya Madaktari hao wakiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi.
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
24/7/2017.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema mfumo wa Madaktari wa Misri wa kuweka utaratibu wa kutoa huduma za Afya kwa Wananchi wa Tanzania umeanza kuleta matumaini kwa Wananchi walio wengi Nchini.
Alisema utaratibu huo unazingatia uhusiano wa muda mrefu wa Kibalozi uliopo kati ya Misri na Tanzania na Zanzibar kwa ujumla ambao ulianza tokea kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika Mwaka 1961 na ule wa Mapinduzi ya Zanzibar wa Mwaka 1964.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akibadilishana mawazo ya Timu ya Madaktari kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha El –Shady kiliopo Alexandria Nchini Misri waliopo Zanzibar kutoa huduma za upasuaji kwa wagonjwa mbali mbali.
Alisema alisema wakati umefika kwa Uongozi wa Vyuo Vikuu tofauti vya Nchini Misri kuzingatia uongezaji wa fursa za masomo ya juu kwa Wanafunzi wa Tanzania hasa katika sekta ya Afya na Elimu.
Balozi Seif alieleza kwamba hatua hiyo itasaidia kwenda sambamba na uimarishaji wa Sera za Afya na Elimu zilizolenga kuimarisha elimu ya Msingi kwa Wanafunzi pamoja na huduma ya afya ya Msingi hasa Vijijini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliueleza Ujumbe huo wa Madaktari Tisa wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha El – Shady Alexandria Nchini Misri kwamba Zanzibar imeweka mkakati wa kuwa na huduma za Afya ya Msingi kila baada ya Kilomita Tano.
Mapema Kiongozi wa Timu ya Madaktari hao kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha El – Shady Alexandria Nchini Misri Profesa Saber Waheeb alisema Timu yake tayari imeshatoa huduma za Afya kwa tariban Mara ya Nnne sasa.
Profesa Waheeb alisema Wataalamu wa Timu hiyo hutoa huduma za upasuaji kwa Watoto walioziba njia ya Mkojo, haja kubwa pamoja na uvimbe wa Tumbo wakitarajia kuwafanyia huduma za Upasuaji wagonjwa wasiopungua 38.
Timu hiyo ya Madaktari Mabingwa wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha El –Shady kiliopo Alexandria Nchini Misri wanamalizia kutoka huduma hizo katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Akiiongoza timu hiyo ya Madaktari Mabingwa wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha El –Shady kiliopo Alexandria Naibu Waziri wa Afya Mheshimiwa Harous Said Suleiman alisema ujio wa Madaktari hao umeleta faraja kwa wagonjwa mbali mbali ambao wangelazimika kutumia gharama kubwa kupata huduma hizo nje ya Nchi.
Naibu Waziri Harous aliushukuru Uongozi wa Chuo cha El –Shady Alexandria Nchini Misri kupitia Hospitali yake kwa uamuzi wake wa kutenga Wataalamu wa Afya kutoa huduma Zanzibar katika mpango endelevu unaofanyika kila kipindi.














No comments:
Post a Comment