TANGAZO


Monday, July 31, 2017

Afisa wa tume ya uchaguzi nchini Kenya aliyetoweka apatikana amefariki

Meneja wa masuala ya teknolojia wa IEBC, alipatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhi maiti mjini Nairobi

Image captionMeneja wa masuala ya teknolojia wa IEBC, alipatikana kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha City mjini Nairobi
Afisa wa cheo cha juu wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, ambaye alitoweka siku ya Ijumaa amepatikana akiwa amefariki.
Chris Musando ambaye ni meneja wa masuala ya teknolojia wa IEBC, alipatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhi maiti mjini Nairobi
Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS na mmoja wa wafanyakazi wenzake.
Kisa hiki kinatokea ikiwa imesalia juma moja kabla ya kuandaliwa uchaguzi mkuu nchini Kenya ambao utafanyika tarehe 8 Agosti.
Polisi wanasema kuwa mwili wa afisa huyo pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la kikuyu lililo vitongoji vya mji wa Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.
Mkurugenzi mkuu wa IEBC Ezra Chiloba (kushoto) akiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City
Image captionMkurugenzi mkuu wa IEBC Ezra Chiloba (kushoto) akiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City
Bwana Musando alikuwa akihusika na usambazaji wa vifaa vyaa eletroniki ambavyo vingetumiwa kutambua wapiga kura na kwa upeperushaji wa matokeo wakati wa uchaguzi mkuu wiki ijayo.
Taarifa zinasema kuwa mwili wa Musando ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City Jumamosi asubuhi na watu waliojitambulisha kuwa polisi.
Mwenyekiti wa IEBC nchini Kenya Wafula ChebukatiHaki miliki ya pichaAFPHaki miliki ya pichaALAMY
Image captionMwenyekiti wa IEBC nchini Kenya Wafula ChebukatiHaki miliki ya pichaAFP

No comments:

Post a Comment