Serikali ya Nigeria imeomba msamaha kwa Saudia baada ya tani 200 za tende kama zawadi ya Ramadhan kupatikana zikiuzwa sokoni nchini humo.
Tende ndio chakula cha kwanza kinachopendwa na Waislamu wakati wa kufungua kila jioni.
Tende hizo zilikuwa zawadi kwa watu waliotoroka majumba yao kutokana na uvamizi wa wapiganaji wa Boko Haram.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Nigeria alisema kuwa uchunguzi unaendelea.
- Boko Haram waanza 'kujisalimisha'
- Ahmad Salkida ahusishwa Boko Haram
- Boko Haram watimuliwa kutoka msitu wa Sambisa
Hatahivyo hakuna mtu aliyekamatwa kufikia sasa.
Wizara ya kigeni imesema kuwa kamishna wa wakimbizi, wahamiaji, pamoja na wakimbizi wa ndani kwa ndani nchini humo alikuwa ametoa orodha ya maeneo ambapo tende hizo zilifaa kupelekwa.
Alikuwa ameorodhesha kambi za wakimbizi wa ndani kwa ndani pamoja na misikiti maarufu.
Tende hizo zilipatikana zikiuzwa katika masoko ya jimbo la Borno, ambalo limeathiriwa vibaya na mzozo huo wa Boko Haram.


No comments:
Post a Comment