Picha ya pamoja ya Wadau wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakar Kambi katika
mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa magonjwa hayo uliyofanyika
Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Wadau kutoka nchi mbali mbali wakifuatilia mjadala kwa ukaribu katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele uliofunguliwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakar Kambi (Hayupo kwenye Picha) uliyofanyika Kunduchi jijini Dar es Salaam. Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Bakar Kambi akiwasilisha mchango wake mbele ya wadau wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (Hawako kwenye picha) katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa wa udhibiti wa magonjwa hayo uliyofanyika Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele Dkt Upendo Mwingira akifuatilia kwa ukaribu mjadala uliokuwa
ukiwasilishwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakar kambi (hayupo kwenye picha)
katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, anaefuatia ni Mkurugenzi wa Idara ya
Afya TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe na Mkurugenzi
wa kinga Dkt. Neema Ruzibamayila.
Na WAMJW, Dar es Salaam
SERIKALI imejidhatiti
kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ili kutimiza malengo ya
kujenga uchumi wa viwanda na afya bora mpaka kufikia 2020.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Mohammed Kambi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka unaolenga kupitia
shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele.
“Tunataka mpaka kufikia 2020 tuwe tumetokomeza
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
kama mabusha na matende ili kuweza kuinusuru nchi katika aina hii ya
magonjwa yanayojitokeza katika nchi zinazoendelea hususan Tanzania” alisema
Prof. Kambi.
Aidha Prof. Kambi amesema kuwa licha ya kudhibiti
mabusha na matende pia wamejidhatiti kuzuia ugonjwa wa usubi na kichocho kabla
ya kufikia 2025 ili kuendana na mpango wa dunia wa kudhibiti magonjwa hayo.
Kwa upande wake Mratibu wa Mpango wa Taifa Wa
kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira amesema
kuwa wananchi wanatakiwa wajitokeze kupata dawa na tiba za magonjwa hayo kwan
hazina madhara kwa binadamu.
Mkutano huo uliokutanisha wadau mbalimbali wa
sekta ya afya kutoka duniani kote umelenga
kupata mpango kazi wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa mwaka
2017 na 2018 ili kuweza kupata njia za kudhibiti magonjwa hayo kama vile
mabusha na matende, kichocho na usubi.

No comments:
Post a Comment