TANGAZO


Sunday, June 18, 2017

Nyota wa muziki Katy Perry afikisha wafuasi milioni 100 katika Twitter

Kate Perry afikisha wafuasi milioni 100 katika Twitter

Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionKate Perry afikisha wafuasi milioni 100 katika Twitter
Msanii wa Marekani Katy Perry amekuwa mtu wa kwanza duniani kupata wafuasi milioni 100 katika mtandao wa Twitter.
Mtandao huo ulichapisha kanda ya video inayoonyesha jumbe zake zote tangu alipojiunga na mtandao huo pamoja na ujumbe unaosema "Today, we #WITNESS history"{Leo #Tumeshuhudia Historia} Witness ni jina la albamu mpya ya Perry.
Mwimbaji wa Canada Justin Bieber ni wa pili kwa idadi kubwa ya wafuasi katika mtandao wa Twitter akiwa na milioni 96.7 naye rais Obama akiwa wa tatu na wafuasi milioni 91.
Ujumbe wa Twitter wa Kate PerryHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionUjumbe wa Twitter wa Katy Perry
Wengine wanaoshirikisha orodha wa watu 100 ni wasanii, wanamichezo, kampuni za habari, na wanasiasa wachache kulingana na mtandao wa Twitter.
Rais wa Marekani Donald Trump ndiye kiongozi anayefuatwa sana aiwa katika nafasi ya 33 baada ya kuwa na wafuasi milini 32.4.
Naye waziri mkuu wa India Narendra Modi akiwa na wafuasi milioni 30.7.

No comments:

Post a Comment