Baadhi ya watoto hao, wakiwa katika kongamano la Watoto, Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Khamis Kigwangalla akiangalia vitabu na vipeperushi alipotembelea mabanda ya taasisi mbalimbali wakati wa kongamano la Watoto, Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi Sihaba Nkinga akisoma kipeperushi katika banda la UNICEF katika kongamano la Watoto, Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk Khamis Kigwangalla akipata maelezo baada ya kutembelea banda la Plan Internaltional katika kongamano la Watoto, Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk Khamis Kigwangalla akionesha Ripoti ya Watoto baada ya kuizindua leo, Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Sihaba Nkinga na Kushoto kwake ni Mwenyekiti Baraza la Watoto, Joel Kiyungu.
Naibu Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk Khamis Kigwangalla, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Sihaba Nkinga na Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Joel Kiyunga wakionyesha Ripoti ya Watoto baada ya kuzinduliwa leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk Khamis Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Sihaba Nkinga, Mwakilishi mkazi wa UNICEF nchini, Bi. Maniza Zaman na Mkurugenzi wa Watoto, Bi. Margareth Mussai katika kongamano la Watoto, Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma. Mkurugenzi wa Watoto, Bi Margareth Mussai akiwa na wabunge wa Viti Maalum, Bi. Fatma Taufiq, Kiteto Koshuma na Bi. Suzan Lyimo katika kongamano la Watoto, Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma.(Picha zote na Daudi Manongi-Maelezo, Dodoma)







No comments:
Post a Comment