Na Judith Mhina - Maelezo
WAZIRI Mkuu Mtaafu na Makamu wa
Kwanza wa Rais, Jaji Joseph Sinde Warioba amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa
kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Madini ya Barrick Prof. John
Thornton juu ya namna Kampuni hiyo itakavyoweza kulipa fedha za madini ambayo
yalikuwa yakisafishwa nje ya nchi kwa njia ya udaganyifu.
Jaji Warioba ametoa pongezi hizo
jana nyumbani kwake Oysterbay, jijini Dar Es Salaam katika mahojiano maalumu na
Idara ya Habari MAELEZO kuhusuiana na hatua iliyochukuliwa na Rais Magufuli
baada ya kupokea taarifa mbili kutoka kwa Kamati alizoziunda kuchunguza mchanga
wenye madini (Makinikia) uliokuwa unasafirishwa kwenda nje ya nchi.
Amesema kwamba, mazungumzo baina
ya Rais na Bwana Thornon ambaye ana hisa kubwa zaidi (64%) katika Kampuni Mama
ya Acacia inayohusika na usafirishaji wa madini kwenda nje ya nchi yamerejesha
imani ya Watanzania juu ya uporwaji wa rasilimali ya nchi uliokuwa unafanywa
kwa miaka mingi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na Kamati ya pili iliyoundwa na Rais Magufuli, thamani ya Makanikia yaliyokuwa
yakisafirishwa kwenda njenya nchi kuanzia mwaka …ni Trilionin 108 fedha za
Kitanzania.
Tuipe nafasi Serikali ifanye
mazungumzo na mmiliki huyo na maamuzi yatakayofikiwa tukubaliane nayo,
tumuamini Rais kwa kile anachokifanya badala ya kuanza kusema , mmiliki huyo
alipe fedha yote ya trilioni 108, hivyo ni kuhukumu kabla ya mazungumzo, ambapo
sio sahihi hata kidogo aliongeza Warioba.
Pia, Jaji Warioba amesema “Watanzania
ni lazima tujiamini kuwa tunaweza, kwa kweli namshukuru sana Rais kwa
kutufumbua macho na kuonyesha njia kuwa watanzania wanaweza kudai haki yao pale
wanapoamua kuisimamia kikamilifu”.
Aidha, Jaji Warioba ameonya tabia
ya baaadhi ya viongozi ya kulalamika yanapojitokeza matatizo ndani ya nchi
badala ya kumsaidia Rais kutafuta ufumbuzi wake akitolea mfano wa suala hili la
Makinikia ambalo wameanza kumlaumu mtu mmoja mmoja. Katika suala kama hili,
kila mtu au Taasisi inatakiwa kumuunga mkono Rais na kumsaidia katika kuhakikisha kwamba rasilimali ya nchi
inalindwa na kutumika kwa manufaa ya Watanzania wote.
“Tatizo la Watanzania tunaangalia
Taasisi au mtu mmoja mmoja. Nashangazwa sana na migawanyiko hii ambayo
inatugawa zaidi badala ya kutufanya wamoja, tusiruhusu hili. Tusiangalie mtu
binafsi, Chama au Taasisi, nadhani ni busara tukasema tumekosea kama Watanzania
na sasa tutoe mawazo ya kujenga na kuboresha utendaji ambao utafanya kila Mtanzania
kufaidika na rasilimali za nchi yetu.” Amesema Jaji Warioba.
“Tutambue kwamba, mfarakano wowote hutokea katika masuala ya
kitaifa kama haya ya rasilimali za nchi, hivyo tusinyosheane vidole tutafute
ufumbuzi wa matatizo yetu kwa pamoja kama nchi kwa masilahi ya vizazi vya sasa
na vijavyo,” alifafanua zaidi Jaji Warioba.
“Namuunga mkono Rais kwa kuwa
amesema angependa kupata maoni kutoka kwa viongozi na watanzania kwa ujumla ni
kwa jinsi gani tunaweza kuboresha hali ya ukusanyaji wa mapato ya madini, mawazo gani yatasaidia kuimarisha Sera,
Sheria, na taratibu kuliko kuendelea na malumbano na kushurutisha kuwaadhibu
viongozi waliopita.” Alisisitiza Waziri Mkuu huyo Msaafu.
Jaji Walioba ambaye amewahi pia
kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais amesema, Rais wetu ni kiongozi ambaye anahitaji
kupata usaidizi wa kutosha kutoka kwetu kama Wananchi na hasa Wasaidizi wake na
Serikali kwa ujumla. “Rais hawezi kufanya kazi peke yake naomba tuimarishe
utendaji wetu wa kazi. Kama utendaji ungekuwa mzuri suala la Makontena kufika
hadi bandarini lisingekuwepo, na hata kugundulika kwake kusingefanywa na
Mheshimiwa Rais,”
Nampongeza sana Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa
utendaji wao wa kazi, ambao ni wasikivu na wanatekeleza kazi zao bila mihemko
wanatoa maagizo na kufatilia kwa wahusika ili watekeleze.
Warioba alimalizia na kusema: “Mara
baada ya Uhuru wa Tanganyika kila mwananchi na viongozi tulilaumu wakoloni kwa kila baya lililokuwa
linatendeka au kutokea, kutokana na hilo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
akasema nanukuu “ Kweli Tanganyika imefikia hapa tulipo kutokana na wakoloni, lakini hatuna budi
kukabiliana na changamoto hizi na kujenga nchi yetu” Mwalimu aliamua kuja na Waraka wa “Act don’t Argue“ na leo hii tumeona changamoto
imetolewa hivyo ni lazima kutoa maoni ili tutoke hapa tulipo sio kunyosheana
vidole.
Sio kweli kwamba hali ilivyo sasa ni mbaya kuliko awamu ya
kwanza au ya pili. Lakini wakati ule kilichotusaidia ni umoja wetu na
mshikamano wa kutatua matatizo yetu kwa pamoja hatukuachiwa kama viongozi
tufanye wenyewe. alihoji Warioba.
Warioba alisisitiza “iweje leo tumuachie Rais afanye kila kitu
mwenyewe naomba sana tumsaidie na kumuunga mkono hakika ana nia njema kabisa na
rasilimali za nchi hii. Ni vema kilichofanyika kikaangalia rasilimali zote za
nchi hii na sio wawekezaji wa nje tu hata wa ndani.
Kwa mfano Tanzanite iko Tanzania pekee lakini biashara
ifanyike Nairobi na New Delhi haya ni mambo ya msingi kuyaona na kuyafatilia.
Wito wangu kwa viongozi inapokuja suala la rasilimali za
taifa tuwe na uongozi wa kitaifa sio chama wala taasisi, wala kukumbusha lipo
ovu au baya lililofanyika Tanzania kwanza Mungu ibariki Tanzania Mungu Mbariki
Rais wetu.


No comments:
Post a Comment