TANGAZO


Thursday, June 15, 2017

Emanuele Palladino:Muacheni Tiote apumzike

Tiote aling'ara vyema akiwa Newcastle

Image captionTiote aling'ara vyema akiwa Newcastle
Wakala wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivori Coast na klabu ya Beijing Enterprises nchini China, Cheick Tiote aliyefariki dunia wiki iliyopita Emanuele Palladino amewataka waandishi wa habari na wadau wa soka kuacha kujadili kifo cha mchezaji huyo.
Tiote alianguka ghafla wakati akifanya mazoezi na klabu yake ya Beijing Enterprises
Image captionTiote alianguka ghafla wakati akifanya mazoezi na klabu yake ya Beijing Enterprises
Ametoa wito na kusisitiza kuwa huu ni wakati wa kuungana na familia ya mchezaji huyo katika maombolezo na kuacha kuendelea kuhoji kifo cha mchezaji huyo.
Mwili wa Tiote unasafirishwa leo kuelekea Ivory Coast
Image captionMwili wa Tiote unasafirishwa leo kuelekea Ivory Coast
Tiote aliagwa siku ya Jumanne na mwili wake ukitarajiwa kurejeshwa nyumbani siku ya leo tayari kwa mazishi.
Papiss Cissé alishindwa kujizuia wakati wa kumuaga Tiote
Image captionPapiss Cissé alishindwa kujizuia wakati wa kumuaga Tiote
Cheick Tiote aliichezea nchi yake mara 52 na kuisaidia kunyakua taji la bara Afrika 2015.

No comments:

Post a Comment