TANGAZO


Saturday, June 17, 2017

Cuba yalaani hatua ya Trump kuiwekea vikwazo upya

Trump

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTrump akiongea huko Miami
Serikali ya Cuba imelaani vikali hatua ya Rais Trump kuiwekea upya vikwazo vya usafiri na biashara taifa hilo baada ya utawala wa Barak Obama kulegeza sheria hiyo, katika harakati ya kuboresha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.
The US embassy in CubaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUbalozi wa Marekani miji Havana
Akiwahutubia wamarekani wenye asili ya Cuba mjini Miami, Trump amesema hatua yake imechangiwa na rekodi ya Cuba ya Ukiukaji wa haki za binadamu hasa, wakati wa utawala wa kidikteta wa Fidel Castro.
Amesema sera hiyo mpya itatilia mkazo sheria juu ya usafiri na kutuma fedha nchini humo.
People walking in HavanaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatu wakitembea mjini Havana
Havana hata hivyo imeskitishwa na uamuzi huo na kuongeza kuwa unarudisha nyuma ushirikiano wa kimaendeleo baina ya mataifa hayo na kwamba Marekani haiwezi kuishauri Cuba juu ya masuala ya haki za binadamu.
Obama and Cuban president Raul Castro took in a baseball game in CubaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionObama na rais wa Cuba Raul Castro 2016

No comments:

Post a Comment