Mtaalam wa Habari na Masoko wa ZIFF, Bi. Lara Presdon akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Tamasha la Filamu za nchi za Majahazi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), Fabrizio Colombo.
Mwenyekiti wa
Taasisi ya Emerson’s Zanzibar Foundation, Said ELG akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu Tuzo ya Filamu itakayotolewa na taasisi yake katika Tamasha la
Filamu za nchi za Majahazi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa
Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), Fabrizio Colombo.
PIX4: Baadhi ya waamdishi wa habari wakifuatilia mkutano wa waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) leo jijini Dar es Salaam.
Na Husna Saidi, Maelezo, Dar es Salaam
19.5.2017
FILAMU
23 za Kitanzania zimefanikiwa kushinda kinyang’anyiro cha filamu bora 132
zitakazoonyeshwa katika tamasha la Nchi
za Jahazi linalotarajia kufanyika Zanzibar kuanzia tarehe 8-16 Julai Zanzibar.
Hayo
yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa Tamasha hilo Fabrizio Combolo wakati
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusu
tamasha hilo ambalo linatarajia kushirika mataifa 70 kutoka sehemu mbalimbali
duniani.
Combolo
alisema filamu zinazotarajiwa kuonyeshwa katika tamasha hilo ni filamu ndefu,
filamu makala, filamu katuni na kwa mara ya kwanza Nchi ya Namibia imeweza
kutayarisha filamu pamoja na filamu ya Winnie iliyotayarishwa kutoka Afrika
Kusini.
“Kutakuwa na makala
kutoka Afrika ya Kusuni yenye jina la Winnie ambayo itazungumzia maisha ya
Winnie Mandera na kwa Tanzania kutakuwa na filamu yenye jina la Kiumeni ambayo
imeshaanza kuonekana katika majumba ya sinema hapa nchini.
Alisema
kutokana na kukua kwa soko la filamu nchini, tamasha hilo kwa mara ya kwanza
litaziduliwa na filamu ya Kitanzania ya T-Junction, iliyotayarishwa na Amil
Shivji, jambo ambalo ni tofauti na huko nyuma ambapo walikuwa wanazindua na
filamu kutoka nje ya nchi.
Aliongeza kuwa
tamasha hilo pia litakuwa na filamu ya makala maalum ya maisha ya Mwanamuziki
wa Marekani, marehemu Winnie Hauston filamu iliyoandaliwa na Mtunzi Nick
Bloomfield.
Aidha Tamasha
hilo pia litaweza kuonyesha filamu ya makala maalum ya Ujangili iliyorekodiwa
hapa nchini ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kupinga vitendo vya ukatili
dhidi ya wanyamapori.
Kwa upande
wake Afisa Habari na Masoko wa tamasha hilo Lara Preston alisema kuwa kwa mara
ya kwanza wameamua kuwa na soko filamu litakalofanyika ndani ya ukumbi huo ili
kutoa hamasa ya kukuza tasnia ya filamu katika Afrika Mashariki.
Nae Mwenyekiti
wa Mfuko wa Emerson, Said Elg alisema kuwa wapo tayari kushirikiana na ZIFF
katika kunyanyua soko la filamu hivyo katika tamasha hilo watatoa tuzo kwa
washindi na kwa wanafunzi 15 kutoka vyuo vya filamu watakaofanya vizuri.
Tamasha hilo
litahusisha tuzo mbalimbali ambazo ni:-Tuzo za nchi za Jahazi, Tuzo za Sembene
Ousmane, Tuzo za filamu bora ya Afrika, Tuzo za Adiaha, Tuzo za filamu bora kwa
wanawake, Tuzo za filamu bora ya Kimataifa, Tuzo za Zanzibar Emerson na Tuzo ya video ya mwanamuziki bora wa Afrika
Mashariki.





No comments:
Post a Comment