Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akipitia taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa
barabara ya Mafinga –Igawa sehemu ya Mafinga –Nyigo KM 74.1 Mkoani Iringa mara
baada ya kukagu mradi huo kulia ni Meneja Mradi huo Richarad Guo akisisitiza
jambo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa ujenzi wa barabara ya Mafinga –Igawa sehemu ya Mafinga –Nyigo KM 74.1 Richarad Guo alipokagua ujenzi huo Mkoani Iringa.
Muonekano wa Barabara ya Mafinga
–Igawa sehemu ya Mafinga –Nyigo KM 74.1 ambapo tayari Kilomita 18 zimekamilika
kwa kiwango cha lami, ujenzi huo unafanywa na kampuni ya China Civil Engenering
Construction Corporation (CCECC).
Mafundi wanaojenga Barabara ya Mafinga-Igawa sehemu ya Mafinga–Nyigo KM 74.1 Mkoani Iringa wakiendelea na ujenzi wa karavati kubwa katika eneo chepechepe maarufu Majinja wilayani Mufindi.
Muonekano wa Mtambo wa kusaga kokoto pamoja na shehena ya kokoto zinazotumika katika ujenzi wa barabara ya Mafinga –Igawa.
NAIBU Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amemtaka mkandarasi China Civil Engeneer
Construction Cooporation (CCECC), anayejenga barabara ya Mafinga-Nyigo km 74.1
na (CRSG) anayejenga sehemu ya Nyigo –Igawa KM 63.8 kuongeza kasi ya ujenzi ili upanuzi na
uimarishaji wa barabara hiyo ukamilike kwa wakati.
Akizungumza mara baada ya kukagua
ujenzi huo Eng. Ngonyani amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa
wa Iringa Eng. Daniel Kindole kuhakikisha upana wa barabara hiyo na ubora wake
unakidhi malengo ya Serikali ili barabara hiyo ili idumu kwa muda mrefu na kupunguza
msongamano na ajali zinazoepukika.
“Barabara hii ambayo ni sehemu ya
barabara kuu ya TANZAM inaunganisha bandari ya Dar es Salaam na nchi za Zambia
na Malawi ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi hivyo ni lazima isimamiwe kikamilifu
ili idumu kwa muda mrefu”, amesisitiza Eng. Ngonyani.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa
barabara hiyo Meneja wa TANROADS Mkoa wa Iringa Eng. Daniel Kindole amesema
tayari kilomita 18 kati ya 74.1 katika sehemu ya kwanza ya Mafinga –Nyigo
imeshawekwa lami na Mkandarasi ameunda
timu tatu ili kuharakisha ujenzi huo.
“Ujenzi wa barabara ya Mafinga -Igawa
unahusisha mikoa mitatu ambapo Kilomita 74.1 ziko katika mkoa wa Iringa
Mafinga-Nyigo, Kilomita 52 ziko katika mkoa wa Njombe Nyigo-Halali na Kilomita
12 ziko katika Mkoa wa Mbeya Halali-Igawa hivyo mimi pamoja na wenzangu
tumejipanga kuhakikisha barabara hii inakamilika Novemba mwakani kama
ilivyopangwa”, amesisitiza Eng. Kindole.
Naye Meneja Mradi wa ujenzi wa
barabara hiyo Sehemu ya Mafinga – Nyigo KM 74.1 Richard Guo amemhakikishia
Naibu Waziri huyo kwamba kasi yao ya ujenzi ni nzuri na barabara hiyo
imeimarishwa ili kukidhi mahitaji na itakamilika kwa wakati.
Zaidi ya shilingi bilioni 116
zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa barabara hiyo sehemu ya kwanza yaani
Mafinga- Nyigo km 74.1 ambazo zinagharamiwa na Serikali ya Tanzania na Benki ya
Dunia.
(Imetolewa na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)

No comments:
Post a Comment